Pata taarifa kuu

Israel yaingia Gaza na vifaru, kabla ya mashambulizi ya ardhini

Israel imetangaza Alhamisi kuwa imeingia katika Ukanda wa Gaza na vifaru, ili "kutayarisha uwanja wa vita" kwa mashambulizi ya ardhini, katika siku ya 20 ya vita vyake dhidi ya Hamas.

Vifaru vya Israeli vimeonekana karibu na mpaka kati ya Israeli na Ukanda wa Gaza, kusini mwa Israeli, Oktoba 20, 2023.
Vifaru vya Israeli vimeonekana karibu na mpaka kati ya Israeli na Ukanda wa Gaza, kusini mwa Israeli, Oktoba 20, 2023. REUTERS - VIOLETA SANTOS MOURA
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hii inayowezekana, iliyoahidiwa mara kwa mara tangu shambulio baya la kundi la wanamgambo wa Hamas kutoka Palestina katika ardhi ya Israel mnamo Oktoba 7, inatia wasiwasi sehemu kubwa ya jumuiya ya kimataifa. "Usiku, jeshi lilifanya mashambulizi na vifaru kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, kama sehemu ya maandalizi yake kwa hatua zinazofuata za mapigano," kulingana na taarifa kutoka kwa msemaji wa jeshi. Askari hao "waliondoka eneo hilo" mwisho wa operesheni, msemaji wa jeqi amebaini.

Kwa mujibu wa picha nyeusi na nyeupe zilizowekwa hadharani na jeshi la Israel, magari ya kivita na tingatinga hupitia kwenye uzio wa ulinzi, sawa na ule unaoitenganisha Israel na Ukanda wa Gaza. Kwa mujibu wa jeshi la Israel, wakati wamashambulizi yao ya usiku, askari "walilenga na kuwapiga magaidi wengi, miundombinu yao na nafasi za kurushia roketi, na kufanya kazi kuandaa uwanja wa vita."

Siku ya Jumatano jioni, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alithibitisha kutayarishwa kwa mashambulizi ya ardhini dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza. "Ni lini, vipi, kiasi gani, na mambo tunayozingatia, siwezi kwenda kwa undani," alisema. Na kama utangulizi wa operesheni hii, jeshi la Israel linashambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza bila kuchoka ambapo Wapalestina milioni 2.4 wamekusanyika pamoja, huku wakizingirwa, huku wakikabiliwa na uhaba wa maji, chakula na umeme.

"Hitilafu"

Mashambulizi ya ardhini yanaonekana kuwa magumu katika eneo hili lenye watu wengi sana, lililojaa mahandaki ambapo Hamas huficha silaha na wapiganaji, na mbele ya mateka zaidi ya 200. Inatia wasiwasi sehemu kubwa ya jumuiya ya kimataifa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitoa uamuzi Jumatano huko Cairo kwamba "mashambulio makubwa" ya ardhini katika Ukanda wa Gaza yatakuwa "kosa". Mwenzake wa Misri, Abdel Fattah al-Sissi, alitoa wito wa kuepuka "uvamizi wa ardhini wa Gaza".

Nchini Marekani, Rais Joe Biden alisema Jumatano kwamba Israel ina "haki" na "wajibu" wa kujilinda lakini lazima ifanye kila linalowezekana "kuwalinda raia wasio na hatia." Bwana Biden, hata hivyo, alihakikisha kwamba "hakuwa amedai" kwamba Bw. Netanyahu acheleweshe uwezekano wake wa mashambulizi hadi kuachiliwa kwa mateka mikononi mwa Hamas.

Takriban mateka 220 walipelekwa Gaza na wapiganaji wa kundi la Hamas, linalotajwa kuwa la kigaidi na Marekani, Israel na Umoja wa Ulaya, kulingana na takwimu kutoka kwa mamlaka ya Israel. Wanawake wanne wameachiliwa huru tangu Ijumaa jioni.

Shambulio la Hamas liliua zaidi ya watu 1,400 nchini Israel, hasa raia, kulingana na mamlaka. Hamas, ambayo imeudhibiti Ukanda wa Gaza tangu mwaka 2007.

Wizara ya Afya ya Palestina imesema kuwa imerekodi vifo zaidi ya 7,000 kufuatia mashambulizi ya anga ya Israel yanayozendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.