Pata taarifa kuu

Israel inaendelea kushambulia kwa makombora kusini mwa Ukanda wa Gaza

Serikali ya Hamas imetangaza kuwa mashambulizi ya Israel yameua takriban watu 80 katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano. Mashambulizi haya pia yamewajeruhi mamia ya watu, ofisi ya vyombo vya habari vya serikali ya Palestina imesema katika taarifa.

Mpalestina akiwa mbele ya jengo lililoharibiwa huko Gaza na mashambulizi yaanga ya Israeli, Oktoba 25, 2023.
Mpalestina akiwa mbele ya jengo lililoharibiwa huko Gaza na mashambulizi yaanga ya Israeli, Oktoba 25, 2023. © Hatem Ali / AP
Matangazo ya kibiashara

Usiku mwingine wa mashambulizi katika maeneo kadhaa ya Palestina. Vikosi vya jeshi la Israel vimesema katika ujumbe uliotumwa kwenye Telegram kwamba wamemuua kamanda wa Hamas usiku wa kuamkia leo Jumatano. Kulingana na jeshi la Israel, kamanda huyo alikuwa ameongoza vikosi vya wanamaji vya Hamas,wameripoti wanahabari wetu maalum huko Jerusalem, Cléa Broadhurst na Boris Vichith. Mashambulizi ya makombora katika Ukanda wa Gaza yameendelea kwa kasi hasa katika saa za hivi karibuni huku jeshi likisema linasubiri operesheni ya ardhini . Israel bado inakataa kuingia kwa mafuta katika eneo la Palestina, ikidai kuwa Hamas bado ina akiba kubwa ya mafuta.

Katika Ukingo wa Magharibi, kuliripotiwa matukio kadhaa, hasa huko Jenin kaskazini mwa Palestina, anasema mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul. Jeshi la Israel liliingia katika kambi ya wakimbizi ya mji huo kwa nguvu ili kukamata baadhi ya washukiwa. Haikuwa rahisi kwa jeshi la Israel kwani lilitaka kutumia nguvu lakini lilijikuta na upinzani mkubwa ambapo pande mbili zilirushiana risase. Hatimaye, jeshi la Israel lilitumia ndege isiyo na rubani kuwaangamiza Wapalestina watatu wenye silaha, kulingana na msemaji wa Israel. Hii inafnya idadi ya vifo kwa zaidi ya watu mia moja waliouawa katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa tangu kuanza kwa vita mnamo Oktoba 7. Katika mwambao wa kaskazini wa Ukanda wa Gaza, maafisa wa kikosi cha wapiga mbizi wa Kipalestina waliangamizwa wakati wa jaribio la kuingia nchini Israel.

Mvutano na nchi jirani

Wakati huu kwenye Miinuko ya Golan kati ya Israeli na Syria. Ndege za Israel zilishambulia maeneo ya Syria. Haya yanafuatia ufyatuaji wa makombora na roketi zilizorushwa na Syria jana jioni. Hii bila shaka ni pamoja na mashambulizi karibu ya kila siku malengo ya makundi yenye silaha yanayoiunga mkono Iran nchini Syria, ambayo yanahusishwa na Israel lakini ambayo kwa hayajawahi kudaiwa na Israeli.

Nchini Lebanon, taarifa kwa vyombo vya habari ya Hezbollah inasema kwamba kiongozi wa kundi hili lenye silaha alikutana na viongozi wa Hamas na Islamic Jihad kujadili njia za kuunga mkono harakati hizi za Wapalestina katika vita vyao na Israel.

Rais wa Uturuki alitoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano kati ya majeshi ya Israel na Palestina. Amesema Uturuki itaendelea kutumia njia zote muhimu za kisiasa, kidiplomasia na kijeshi. Wakati huo huo rais wa Uturuki alielezea Hamas kama kundi la ukombozi linaloendesha vita kulinda ardhi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.