Pata taarifa kuu

Pakistan: Watu kadhaa wauawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mlipuko

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, watu wasiopungua 52 wameuawa na zaidi ya wengine 65 wamejeruhiwa, leo Ijumaa, Septemba 29, wakati wa shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya mkutano wa kidini katika jimbo la Balouchistan, kusini magharibi mwa Pakistan. Idadi ya vifo inaendelea kuongezeka.

Waathiriwa wanatibiwa katika Hospitali ya Mastung kufuatia shambulio baya la kujitoa mhanga wakati wa mkutano wa kidini katika mkoa wa Balutchistan huko Pakistan mnamo Septemba 29, 2023.
Waathiriwa wanatibiwa katika Hospitali ya Mastung kufuatia shambulio baya la kujitoa mhanga wakati wa mkutano wa kidini katika mkoa wa Balutchistan huko Pakistan mnamo Septemba 29, 2023. © Shaheed Nawab Ghous Bakhsh Raisa / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya eneo hilo imehusisha mlipuko huo kwa shambulio la kujitoa mhanga. Mlipuko huo ulitokea Ijumaa, Septemba 29, karibu na msikiti, wakati umati wa waumini walikusanyika kwa maandamano ya kuashiria siku ya kuzaliwa kwa Mtume wa Muhammad (S.A.W). Maadhimisho haya yanakubaliwa na madhehebu mengi ya Waislamu, lakini mengine yanalaani.

"Mamia ya mamia ya watu walitoka kwenye msikiti wa Madina, na walipoingia kwenye Barabara ya Al Falah, mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua katikati ya umati," amesema Abdul Razzaq Sasoli, afisa wa utawala wa eneo hilo.

Huko Karachi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Pakistani imethibitisha mlipuko uliosababishwa na "magaidi". "Shambulio dhidi ya watu wasio na hatia ambao walikuwa wanashiriki katika hafla ya  Mawlid ni kitendo kiovu," wizara hiyo imesema katika taarifa. Waathiriwa wanatibiwa katika hospitali moja katika mji  jirani wa Mastung.

Wito wa michango ya damu

Hakuna kundi lililoodai kuhusika na shambulio hilo, ambalo linaingilia kati katika muktadha wa kuibuka tena kwa mashambulio yaliyodaiwa na makundi ya wanamgambo magharibi mwa nchi, wakati uchaguzi umepangwa kufanyika mnamo mwezi Januari 2024. Taliban wa Pakistani wamebaini kwamba hawahusiki katika shambulio la Ijumaa. "Tehrik-e-Taliban Pakistan haina uhusiano wowote na shambulio hili, na ndio msimamo wetu juu ya shambulio la bomu katika maeneo ya umma ," kundi hilo limesema.

Waziri wa Habari wa Balouchistan, Jan Achakzai alitaka michango ya damu kutibu waliojeruhiwa. Aliamuru pia kufanya maombolezo ya siku tatu. Kila mwaka kwa tarehe hii, misikiti na majengo ya serikali nchini Pakistan huangaziwa, wakati waumini huandamana wakati wa maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mtume.

Mnamo Aprili 2006, shambulio la mshambuliaji wa kujitoa mhanga dhidi ya maandamano ya waumini wa madhehebu ya Sunni kuashiria tukio hilo lilisababisha vifo vya  watu wasiopungua 50 katika mji wa Karachi. Shambulio hilo halijawahi kudaiwa, lakini wanaume watatu kutoka kwa kundi la Lashkar-e-Jhangvi walinyooshewa kidole cha lawama. Balouchistan ni nyumbani kwa vmakundi kadhaa yanayotaka kujitenga kwa maeneo yao.

(Pamoja na mashirika)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.