Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Mapigano yazuka kati ya wanajeshi na 'mamia' ya Taliban karibu na mpaka wa Afghanistan

Tehreek-e-Taliban Pakistan ilianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya jeshi la Pakistan Jumatano hii alfajiri. Mapigano hayo yaliyochukua muda wa saa nne yalizuka katika wilaya ya Chitral, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa.

Taliban wa Pakistani wa TTP mwaka 2012.
Taliban wa Pakistani wa TTP mwaka 2012. AP - Ishtiaq Mahsud
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wa Pakistani, wakisaidiwa na vikosi vya ziada vilivyotumwa katika eneo la mpakani, walizuia shambulio kutoka Afghanistan lililokuwa likiendeshwa na "mamia" ya Taliban ya Pakistan siku ya Jumatano, afisa mkuu amesema. Mamia ya wapiganaji wa TTP, Tehreek-e-Taliban Pakistan waliokuwa na silaha nyepesi na nzito walilenga vituo viwili vya kijeshi vilivyoko Kalash katika wilaya ya Chitral.

Kamanda wa TTP anadai katika taarifa yake kuteka vijiji kadhaa, vituo viwili vya kijeshi katika eneo la Bomburit na kwamba wanajeshi sita wa Pakistani waliuawa na kundi lake katika majibizano ya risasi. Naibu mkuu wa polisi katika wilaya hiyo anathibitisha vifo vya askari wanne na "magaidi kumi na wawili walitumwa motoni". Habari ambayo haikuweza kuthibitishwa.

Kuongezeka kwa mashambulizi

Shambulio hilo lilitekelezwa siku ambayo Pakistan inaadhimisha Siku ya Ulinzi ambayo inaashiria dhabihu ya wanajeshi wa Pakistani ambao waliuawa mashujaa kwa ulinzi wa mipaka. Njia ya TTP, iliyotiwa moyo na kurejea madarakani kwa Taliban nchini Afghanistan, kuikumbusha serikali ya Pakistani kwamba haitaachana na vita vyake vya kuweka sheria ya Kiislam (Sharia) na kuliangusha jeshi ambalo inasema kuwa ni la uzushi.

Taliban waa Pakistani wanashiriki itikadi kali ya Kiislamu na wenzao wa Afghanistan. Kundi hilo lilianzishwa mwaka 2007, wakati wanamgambo wanaopigana pamoja na Taliban nchini Afghanistan walipojitenga na kuelekeza uasi wao dhidi ya Islamabad. Wakati wa miezi 12 ya kwanza ya utawala wa Taliban nchini Afghanistan, Pakistan ilishuhudia ongezeko la 50% la mashambulizi ya wanamgambo wa Kiislamu, wanaopiga kambi katika mikoa ya mpaka wa magharibi, kulingana na Taasisi ya Pak Institute for Peace Studies (PIPS).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.