Pata taarifa kuu

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan amekamatwa

Waziri wa zamani wa Pakistan Imran Khan amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa tuhuma za rushwa.

Imran Khan,waziri mkuu wa zamani wa Pakistan
Imran Khan,waziri mkuu wa zamani wa Pakistan AP - K.M. Chaudary
Matangazo ya kibiashara

Mahakama nchini humo imekuta kiongozi huyo wa zamani na kosa la kutotangaza pesa alizopata kutokana na kuuza zawadi za serikali. 

Khan kwa upande wake amekanusha mashtaka akisema kuwa atakata rufaa. Tayari kiongozi huyo amekamatwa kwa amri ya mahakama.

Polisi wamemchukua kiongozi huyo nyumbani kwake baada ya mahakama kuagiza afungwe
Polisi wamemchukua kiongozi huyo nyumbani kwake baada ya mahakama kuagiza afungwe © K.M Chaudary / AP

Waziri mkuu huyo wa zamani aliyechaguliwa mwaka wa 2018, aliondolewa madarakani baada ya kupigwa kwa kura ya kutokuwa na imani naye mwaka wa 2022.

Khan alikamatwa mwezi Mei kwa kutofika mahakamani kama ilivyotakiwa kabla ya kuachiwa huru na kisha baadae kukamatwa tena.

Awali maandamano yalishuhudiwa nchini humo baada ya kukatwa kwa kiongozi huyo wa zamani
Awali maandamano yalishuhudiwa nchini humo baada ya kukatwa kwa kiongozi huyo wa zamani AFP - ASIF HASSAN

Maandamano makubwa yalishuhudiwa nchini humo, wafuasi wake wakipinga hatua ya kukamatwa kwa kiongozi wao.

Kupitia kwa ujumbe wa sauti uliorekodiwa kabla ya kukamatwa kwake, Khan amewataka wafuasi wake kuwa watulivu akisema kwamba alifanya hivyo akijuwa kwamba atakamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.