Pata taarifa kuu

Pakistan: Waziri mkuu wa zamani Imran Khan ameondolewa mashtaka ya ufisadi

Nairobi – Mahakama nchini Pakistan, imeondoa mashtaka ya ufisadi dhidi ya waziri mkuu Imran Khan na kuagiza kuchiwa kwake huru kwa dhamana. 

Msemaji wa chama chake cha Pakistan Tehreek-e-Insaf, amethibitisha kufutwa kwa hukumu hiyo
Msemaji wa chama chake cha Pakistan Tehreek-e-Insaf, amethibitisha kufutwa kwa hukumu hiyo AP - K.M. Chaudary
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja, baada ya kuhukumiwa jela miaka mitatu na Mahakama nyingine, Agosti tarehe 5 kwa kosa la kutpoweka wazi mali zake, na kuuza zawadi za serikali, wakati akiwa Waziri Mkuu kati ya mwaka 2018 hadi 2022. 

Hata hivyo, Wakili wake amesema haijawa wazi iwapo Khan ataachiwa huru mara moja baada ya uamuzi huo wa Mahakama, na kuwa wasiwasi kuwa huenda akakamatwa tena kwa sababu kuna kesi nyingine zaidi ya 200 dhidi yake. 

Msemaji wa chama chake cha Pakistan Tehreek-e-Insaf, amethibitisha kufutwa kwa hukumu hiyo, ambayo pia ilikuwa imemzuia kuwania tena uongozi wa nchi hiyo. 

Khan mwenye umri wa miaka 70, hata kabla ya kuhukumiwa jela, alikanusha madai dhidi yake na kusema, analegwa kisiasa ili kumzuia, kutafuta tena uongozi wa nchi hiyo, baadaye mwaka huu. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.