Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Syria: Watu 20 wauawa katika makabiliano kati ya FDS na makabila ya Kiarabu

Kwa siku ya 8 mfululizo, mapigano yanaendelea mashariki mwa Syria kati ya Syrian Democratic Forces (SDF) inayotawaliwa na Wakurdi na makabila ya Kiarabu. Watu 20 wameuawa siku ya Jumanne, kulingana na shirika laHaki za Kibinadamu nchini Syria, na kufanya idadi ya vifo katika mapigano haya kati ya washirika kufikia 90.

Mwanajeshi wa FDS mnamo Septemba 4, 2023.
Mwanajeshi wa FDS mnamo Septemba 4, 2023. AFP - DELIL SOULEIMAN
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kikanda, Paul Khalifeh

Mapigano hayo yamejikita karibu na mji wa Zeiban, kwenye ukingo wa kushoto wa Euphrates, ngome ya kiongozi wa kikabila Ibrahim al-Hafl, anayechukuliwa na wapiganaji wa Syrian Democratic Forces (SDF) kama mchochezi wa uasi wa makabila ya Kiarabu. Kituo cha Kiarabu cha al-Mayadeen, kilio na ushirikiano wa karibu na Damascus, kinaonyesha kuwa SDF ilishambulia kwa nguvu mji wa Zeiban kwa kutumia ndege zisizo na rubani na makombora mbalimbali.

Licha ya kuwa na silaha kubwa zaidi kuliko wapiganaji wa kikabila, vikosi vinavyotawaliwa na Wakurdi vinaendelea kusonga mbele polepole. Makabila ya Waarabu, ambayo yametangaza uhamasishaji wa jumla, yanaweka upinzani mkali.

Shirika la Haki za Kibinadamu nchini Syria na vyanzo vilivyo karibu na Damascus vinasema kuwa SDF wameteka tena baadhi ya maeneo baada ya kuleta idadi kubwa ya wapiganaji kutoka majimbo mengine yaliyo chini ya udhibiti wao. Lakini sehemu nzuri ya mashariki mwa mkoa wa mashariki wa Deir Ezzor bado hawajaipatia kuidhibiti.

Mazungumzo na wakimbizi

Maafisa na wanadiplomasia wa Marekani walifadhili mkutano kati ya wawakilishi wa wapiganaji kujaribu kuzuia mapigano kati ya washirika wao. Upatanishi umeshindwa.

Kutokana na ghasia hizo, wakaazi wa maeneo kadhaa walivuka hadi kwenye ukingo wa kulia wa Euphrates kupata hifadhi katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali ya Syria.

Kwa zaidi ya wiki moja, FDS na makabila ya Kiarabu wamekuwa yakizozana kufuatia kukamatwa kwa Ahmad al-Khabil, aliyekuwa mkuu wa Baraza la Kijeshi la Deir Ezzor, kundi la Warabu wenye silaha linaloshirikiana na FDS. Kundi hili linatuhumiwa kwa ubadhirifu, ulanguzi wa dawa za kulevya na kula njama dhidi ya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.