Pata taarifa kuu

Wanajeshi wanne wa Syria wameuawa katika shambulio la Israeli

Wanajeshi wanne wa Syria na wapiganaji wawili wanaoungwa mkono na Iran wameuawa mapema leo Jumatatu na wanajeshi wa  Israeli karibu na Damascus, kwa mujibu wa taarifa ya shirika la ufuatiliaji wa vita.


Israel imekuwa ikitekeleza mashambulio nchini Syria dhidi ya kile inachosema ni kulenga ngome za kijeshi za Iran na Hezbollah © AFP
Israel imekuwa ikitekeleza mashambulio nchini Syria dhidi ya kile inachosema ni kulenga ngome za kijeshi za Iran na Hezbollah © AFP AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Hili limetajwa kuwa shambulio la hivi karibuni la anga kutekelezwa na wanajeshi wa Israel katika mji mkuu wa Syria ulioharibiwa na vita.

Mashambulio hayo ya anga yalilenga vikosi vya serikali ya Syria, na ngome za kijeshi na ghala za silaha zinazotumiwa na makundi yenye silaha yanayoungwa mkono na Tehran, kulingana na Shirika la kufuatilia haki za binadamu la Syria.

Wakati wa zaidi ya muongo mmoja wa vita nchini Syria, taifa jirani la Israel limetekeleza mamia ya mashambulio ya anga katika ardhi yake, yakilenga vikosi vinavyoungwa mkono na Iran na wapiganaji wa Hezbollah pamoja na maeneo ya jeshi la Syria.

Rami Abdel Rahman, mkuu wa kitengo cha uchunguzi katika shirika ufuatiliaji wa vita, amesema kwamba "wanajeshi wanne wa Syria akiwemo afisa mmoja, pamoja na wapiganaji wawili wanaoungwa mkono na Iran waliuawa katika mashambulio ya anga kwenye maeneo ya makundi yanayoungwa mkono na Tehran na maghala ya risasi na silaha."

Mashambulio  hayo ya Israel yamelenga maeneo karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damascus, uwanja wa ndege wa Dimas na Kisweh, karibu na mji mkuu, na kuharibu maghala ya silaha na risasi za makundi yanayoungwa mkono na Iran, lilisema shirika hilo lenye makao yake makuu nchini Uingereza ambalo linategemea mtandao mpana ndani ya Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.