Pata taarifa kuu

Ghala la kombora lalipuka karibu na Damascus

Ghala lililolengwa ni la wanamgambo wanaounga mkono Iran, wanaochukuliwa kuwa washirika wa utawala wa Bashar Al-Assad. Hili ni shambulio la pili kwa wiki.

 Rais wa Syria Bashar Al-Assad.
Rais wa Syria Bashar Al-Assad. AFP
Matangazo ya kibiashara

Ghala la kuhifadhia makombora la wanamgambo linalofikiriwa kuwa linaunga mkono Iran lililipuka sana Jumapili hii, Agosti 13 mapema asubuhi. Tukio hili, lililo karibu na Damascus, mji mkuu wa Syria, lilisababisha uharibifu wa nyenzo kulingana na Shirika la Kuchunguza Haki za Kibinadamu la Syria (OSDH).

"Mlipuko wa kutisha" uliyosikika na wakaazi wa Damascus na viunga vyake ulitokea katika "maghala ya wanamgambo wanaoiunga mkono Iran", washirika wa serikali ya Syria, katika eneo la milima mashariki mwa mji mkuu, limeongeza shirika hilo. "Hatujui kama ni shambulio la anga au operesheni ya ardhini," amesema Rami Abdel Rahmane, mkurugenzi wa OSDH yenye makao yake makuu nchini Uingereza na ambaye ana mtandao mpana wa vyanzo nchini Syria.

Kwa upande wake, shirika rasmi la Sana lilikuwa limeonyesha wakati wa usiku kwamba "sauti za milipuko" zilisikika "nje kidogo ya Damascus", bila kutaja sababu.

Israel ilishambulia tarehe 7 Agosti

Siku ya Jumatatu, mashambulizi ya Israel kwenye maeneo ya kijeshi na maghala ya silaha nje kidogo ya Damascus yalisababisha vifo vya wanajeshi wanne wa Syria na wapiganaji wawili wanaoiunga mkono Iran, kulingana na OSDH.

Wanajeshi wawili wa Syria na wapiganaji watano wa kigeni pia walijeruhiwa katika uvamizi huo ulioharibu maghala ya silaha na risasi za wanamgambo wanaoiunga mkono Iran, washirika wa utawala wa Syria, hasa karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damascus. Israel haijato maoni yoyote juu ya mashambulizi haya lakini inasema inataka kuzuia Iran kujiimarisha kwenye milango yake.

Mnamo Julai 19, wapiganaji watatu wanaounga mkono serikali waliuawa na wanne kujeruhiwa katika mashambulizi ya usiku ya Israeli dhidi ya maeneo ya jeshi na makundi yanayounga mkono Iran karibu na Damascus, kulingana na OSDH.

Israel pia ililenga kambi ya ulinzi wa anga katika jimbo la pwani la Tartus, kulingana na chanzo hicho. Tangu kuanza kwa vita nchini Syria mwaka 2011, Israel imefanya mamia ya mashambulizi ya angani dhidi ya nyadhifa za utawala wa Syria pamoja na vikosi vya Iran na kundi la Hezbollah la Lebanon linaloiunga mkono Iran, washirika wa Damascus na kuwaapisha maadui wa Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.