Pata taarifa kuu

Ziara ya Assad katika Umoja wa Falme za Kiarabu: Damascus kujiunga tena na nchi za Kiarabu

Hii ni ziara ya pili ya rais wa Syria katika Ghuba tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi nchini Syria. Baada ya ziara katka nchi ya Oman mwezi uliopita, Bashar Al-Assad, amepokelewa Jumapili hii, Machi 19 katika Umoja wa Falme za Kiarabu na Rais Mohammed ben Zayed. Ishara mpya ya kuimarika kwa mawasiliano kati ya Damascus na nchi za Kiarabu.

Rais wa Syria Bashar al-Assad (kushoto) akilakiwa kwenye uwanja wa ndege na Rais wa Falme za Kiarabu, Sheikh Mohammed bin Zayed Al-Nahyan, mjini Abu Dhabi, Machi 19, 2023.
Rais wa Syria Bashar al-Assad (kushoto) akilakiwa kwenye uwanja wa ndege na Rais wa Falme za Kiarabu, Sheikh Mohammed bin Zayed Al-Nahyan, mjini Abu Dhabi, Machi 19, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu katika Ghuba, Nicolas Keraudren

Ziara hii mpya ya rais wa Syria katika Umoja wa Falme za Kiarabu ni hatua moja zaidi ya 'kurudi' kwa Damascus kwenye "jumuiya ya nchi za KIrabu ". Kwa vyovyote vile, hivi ndivyo Anwar Gargash, mshauri wa kwanza wa Rais wa Imarati Mohamed bin Zayed, amesema leo kwenye ukurasa wake wa Twitter. Mbinu hii, ameongeza, "ni sehemu ya maono ya kina […] yenye lengo la kuimarisha utulivu wa nhi za Kiarabu na kikanda".

Kwa miaka michache sasa, Abu Dhabi imekuwa ikiongeza juhudi za kidiplomasia kwa Syria. Utawala wa Ghuba, kwa mfano, ulifungua tena ubalozi wake huko Damascus mwishoni mwa 2018. Kumbuka pia kwamba Bashar Al-Assad alisafiri kwenda Imarati mwaka mmoja uliopita: ziara yake ya kwanza katika nchi ya Kiarabu tangu 2011.

Kwa hivyo upatanisho unaonekana kuwa mzuri na umepiga hatua chanya. Washirika wengine wa Abu Dhabi katika Ghuba wanaweza kufuata mkondo huo. Mwezi uliopita, waziri wa mambo ya nje wa Saudia alisema mbinu mpya ya Syria inahitajika ili kukabiliana na mzozo wa kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.