Pata taarifa kuu
GENEVA-URUSI-MAREKANI-SYRIA

John Kerry na Sergei Lavrov wakubaliana kukutana tena kuzungumzia Syria

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Marekani na Urusi hii leo wamekubaliana kukutana tena kwa mara ya pili ndani ya majuma mawili yajayo kupanga tarehe rasmi ya kuanza kwa mazungumzo ya amani kuhusu Syria mjini Geneva Uswis. 

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov na mwenzake wa Marekani John Kerry wakipeana mikono kupongezana
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov na mwenzake wa Marekani John Kerry wakipeana mikono kupongezana Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry amewaambia waandishi wa habari hii leo mjini Geneva kuwa yeye na mwenzake wa Urusi wamekubaliana kimsingi kukutana tena majuma mawili yajayo kupanga tarehe ya kuanza kwa mazungumzo mapya kuhusu Syria.

Awali mazungumzo yaliyokuwa yamepangwa kufanyika mjini Geneva yalivunjika baada ya kutumika kwa silaha za kemikali nchini Syria, uamuzi ambao ulichangiwa kwa sehemu kubwa na nchi ya Marekani kujiondoa.

Kwenye mazungumzo yao mjini Geneva, waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov, amesema kuwa mazungumzo yao yamekuwa ya mafanikio na kwamba mambo ya msingi kuhusu Syria watayajadili wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa mwezi ujao.

Kwenye mkutano wao na waandishi wa habari, pia alikuwepo mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu kwa nchi ya Syria, Lakhdar Brahimi ambaye amepewa jukumu lakuhakikisha amani inapatikana nchini Syria.

Brahimi amesema kuwa anamatumaini jumuiya ya kimataifa hasa nchi za Urusi na Marekani zitafikia makubaliano ya pamoja kuhusu njia bora ya kumaliza machafuko ya nchini Syria huku akionesha kutounga mkono kuchukuliwa kwa hatua zozote za kijeshi dhidi ya Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.