Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Syria: Wanajeshi wanane wa serikali wauawa katika shambulio la wanajihadi

Wanajeshi wanane wa Syria wameuawa siku ya Jumatano katika shambulio la kundi la wanajihadi la Hayat Tahrir al-Cham (HTS), tawi la zamani la mtandao wa Al-Qaeda nchini Syria, kaskazini-magharibi mwa Syria, kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu nchini Syria (OSDH).

Wanajeshi wa Syria katika mkoa wa Hama, Syria, mwaka 2015.
Wanajeshi wa Syria katika mkoa wa Hama, Syria, mwaka 2015. AP - Alexander Kots
Matangazo ya kibiashara

"HTS imerusha makombora na roketi kwenye kituo cha jeshi la Syria na kuua wanajeshi wanane karibu na Kafr Rouma, katika jimbo la Idlib," limesema shirika hilo lisilo la kiserikali, lenye makao yake makuu nchini Uingereza na ambalo lina mtandao mpana wa vyanzo nchini Syria.

Vyombo vya habari vya serikali ya Syria havikuripoti shambulio hilo mara moja.

Tangu mwishoni mwa mwaka 2022, HTS "imezidisha mashambulizi yake" dhidi ya ngome za jeshi la utawala wa Bashar al-Assad huko Idleb, baada ya maelewano kati ya Ankara na Damascus, kulingana na mkurugenzi wa OSDH, Rami Abdel Rahman.

Syria na Uturuki, ambayo inaunga mkono waasi wa Syria, zimeanza tena mazungumzo baada ya mpasuko uliodumu kwa zaidi ya muongo mmoja kufuatia vita vya mwaka 2011 nchini Syria.

Mkutano wa pande tatu ulifanyika mnamo mwezi Desemba huko Moscow kati ya mawaziri wa ulinzi wa Uturuki, Syria na Urusi, ikiwa ni mkutano wa kwanza tangu 2011.

Usitishaji mapigano tangu mwezi Machi 2020

Uturuki ilianzisha mashambulizi matatu katika ardhi ya Syria tangu mwaka 2016 dhidi ya majeshi ya Wakurdi kaskazini mwa nchi hiyo, ambayo yameiwezesha kudhibiti ukanda wa mpaka wa Syria, "kitendo" kilicholaaniwa na Damascus.

Takriban nusu ya mkoa wa Idlib na maeneo yanayopakana na mikoa jirani ya Hama, Aleppo na Latakia yanatawaliwa na HTS na makundi ya waasi yenye ushawishi mdogo.

Licha ya mapigano ya hapa na pale, makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyopendekezwa na Moscow, mshirika wa Damascus, na Ankara, yameheshimiwa kwa kiasi kikubwa tangu mwezi Machi 2020 katika ukanda huu.

Vita nchini Syria vimeua takriban watu nusu milioni tangu mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.