Pata taarifa kuu
SYRIA- USALAMA-CHAKULA

UN imeongeza muda wa zoezi la utoaji misaada ya kibinadamu nchini Syria

Baraza la usalama la umoja wa Mataifa, hapo jana limeongeza muda wa miezi 6 zaidi wa zoezi la utoaji misaada ya kibinadamu nchini Syria, muda ambao hata hivyo baadhi ya nchi wanachama wanauona mdogo.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa
Baraza la usalama la umoja wa mataifa REUTERS - DAVID DEE DELGADO
Matangazo ya kibiashara

Azimio hili linalenga kufikisha misaada hitajika kwa mamilioni ya raia kaskazini mwa Syria ambao wanakabiliwa na hali mbaya.

Barabara Woodward ni balozi wa Uingereza kwenye umoja wa Mataifa.

“Raia milioni moja na laki nne wa Syria wanategemea misaada ya chakula na dawa inayotolewa chini ya mpango huu.”Ameeleza Barabara Woodward.

Mataifa mengi ya dunia yanaendelea kukabiliwa na kipindi kigumu haswa wakati huu nchi zinapokabiliwa na changamoto za baada ya uviko 19, mfumuko wa bei za bidhaa, vita vya Ukraine pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.