Syria: UN yaona masharti ya Damascus kupitisha misaada mpakani 'hayakubaliki'
Umoja wa Mataifa una wasiwasi kuhusu 'masharti yasiyokubalika' yaliyotolewa na Damascus kutumia kivuko cha mpaka cha Bab al-Hawa kupeleka misaada ya kibinadamu katika maeneo ya waasi kaskazini magharibi mwa Syria, kulingana na waraka ambao uliosomwa na shirika la habari la AFP siku ya Ijumaa.
Imechapishwa:
Barua kutoka kwa mamlaka ya Syria inayoruhusu utumiaji wa sehemu hii ya mpakani kati ya Uturuki na Syria "ina masharti mawili yasiyokubalika", imebaini hati iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama siku ya Ijumaa na Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) , ambayo inasema ina wasiwasi kuhusu marufuku yaliyowekwa kuzungumza na mashirika "yaliyotajwa kama 'magaidi'" na "usimamizi" wa shughuli zake na mashirika mengine.