Pata taarifa kuu

Baraza Kuu la UN launda chombo cha 'kufafanua' hatima ya watu waliotoweka Syria

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeunda "taasisi huru" mnamo Alhamisi Juni 29 "kufafanua" hatima ya maelfu ya watu ambao wametoweka nchini Syria kwa miaka 12.

Sehemu ya ndani katika gereza la Aleppo, Syria, Mei 22, 2014.
Sehemu ya ndani katika gereza la Aleppo, Syria, Mei 22, 2014. AFP - HO
Matangazo ya kibiashara

Hili lilikuwa ombi la mara kwa mara kutoka kwa familia na watetezi wa haki za binadamu.

Wakati, kwa mujibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali, takriban watu 100,000 wametoweka tangu kuzuka kwa vuguvugu la wananchi mwaka 2011, azimio hilo linaamua kuanzisha "chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, Taasisi Huru ya Watu Waliotoweka ya Jamhuri ya Kiarabu ya Syria, kufafanua hatima na mahali walipo watu wote waliotoweka” nchini Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.