Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Lebanon: Makabiliano makali yaendelea katika kambi ya Wapalestina ya Aïn el-Heloué

Kwa siku ya tatu mfululizo, kambi ya Wapalestina ya Aïn el-Héloué, iliyoko kilomita 40 kutoka mji mkuu wa Lebanon, Beirut, ilikumbwa  na makabiliano makali siku ya Jumatatu kati ya chama cha Fatah la Rais Mahmoud Abbas na makundi ya Kiislamu yenye itikadi kali, ambayo yamesababisha vifo vya watu kumi na moja na mamia kadhaa kujeruhiwa.

Wapiganaji wa Fatah wanaharakia kupiga kambi  katika kambi ya Aïn el-Héloué, Julai 31, 2023, nchini Lebanon.
Wapiganaji wa Fatah wanaharakia kupiga kambi katika kambi ya Aïn el-Héloué, Julai 31, 2023, nchini Lebanon. AP - Mohammad Zaatari
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Beirut, Paul Khalifeh

Mashambulizi kadhaa yaliyoanzishwa na wapiganaji wa Fatah dhidi ya ngome za makundi ya Kiislamu, hasa katika sehemu ya kaskazini ya kambi hiyo, yalisababisha karibu 60% ya wakaazi wake 60,000 kuyatoroka makazi yao siku ya Jumatatu.

Licha ya makabiliano makali kwa makombora, roketi na silaha zingine za kivita, yote hayo hayajabadilisha chochote katika uwanja wa mapigano. Mapigano hayo yalienea hadi katika mji jirani wa Saida, ambapo shule, biashara na ofisi za serikali zlifungwa kufungwa.

Makundi mbalimbali ya Kiislamu yameungana kukabiliana na Fatah, ambayo inaonekana imedhamiria kulipiza kisasi mauaji ya siku ya Jumapili ya kiongozi wake na walinzi wake watatu.

Jeshi la Lebanon, ambalo liko karibu na kambi hiyo, limeimarisha hatua zake za usalama na kuleta vitengo mbalimali vya wanajeshi.

Uingiliaji kati katika kambi ya Aïn el-Héloué hauwezekani, hata hivyo, kwani usalama ndani ya kambi unasimamiwa na Fatah, kulingana na makubaliano yaliyohitimishwa miaka 50 iliyopita kati ya Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina na serikali ya Lebanon.

Mapigano hayo yamesababisha uharibifu mkubwa kwa nyumba na biashara katika kambi hiyo. Mitaa imejaa uchafu na moshi mkubwa umefumba katika vitongoji vyenye makazi.

Hata hivyo pande mbili zinazokinzana zilifikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano, kwa juhudi za mbune wa Lebanon kutoka mji wa Saida, Oussama Saad.

Lakini mapigano ya hapa na pale yameendelea hadi usiku wa manane licha ya kusitishwa kwa mapigano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.