Pata taarifa kuu

Mahmoud Abbas wa Palestina na Netanyahu wa Israeli kuzuru Uturuki

Nairobi – Kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu watazuru Uturuki baadaye mwezi huu kufanya mazungumzo na Rais Recep Tayyip Erdogan.

Viongozi hao wanatarajiwa kuzuru Uturuki katika nyakati tofauti
Viongozi hao wanatarajiwa kuzuru Uturuki katika nyakati tofauti REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Netanyahu atawasili nchini humo Julai 28, siku chache baada ya Abbas, ambaye anatarajiwa kuzuru Julai 25, ofisi ya rais wa Uturuki ilisema.

Viongozi hao watajadili "uhusiano wa Uturuki na Palestina na maendeleo ya hivi punde katika mzozo wa Israel na Palestina, pamoja na masuala mengine muhimu ya kimataifa", iliongeza taarifa hiyo ya Uturiki.

Ziara ya Netanyahu itakuwa ya kwanza kufanywa na waziri mkuu wa Israel tangu Ehud Olmert mwaka 2008.

Ziara hii inakuja wakati Israeli na Palestina zikionekana kukabiliana
Ziara hii inakuja wakati Israeli na Palestina zikionekana kukabiliana REUTERS - AMIR COHEN

Uhusiano kati ya Uturuki na Israel umeimarika katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, kwa ziara kadhaa za ngazi ya juu, ikiwa ni pamoja na ile ya Rais wa Israel Isaac Herzog baada ya zaidi ya muongo mmoja wa mvutano.

Mnamo mwaka wa 2010, uhusiano ulidorora baada meli ya Uturuki kushambuliwa na makomando wa Israel na kusababisha kuwepo kwa uhusiano mbaya kwa zaidi ya nusu ya muongo.

Uturuki ilimwita balozi wake nchini Israel mwezi Mei 2018, na kumfukuza balozi wa Israel nchini Uturuki baada ya Wapalestina wapatao 60 kuuawa na wanajeshi wa Israel huko Gaza wakati wa maandamano dhidi ya Israel kuzingira eneo la pwani kinyume cha sheria.

Roketi zarushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israeli, huko Gaza, Jumatano, Mei 10, 2023.
Roketi zarushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israeli, huko Gaza, Jumatano, Mei 10, 2023. AP - Hatem Moussa

Erdogan aliishutumu Israel kwa "ugaidi" kutokana mauaji hayo  na kuliita taifa  hilo kama la kibaguzi.

Israel ililipiza kisasi kwa kumfukuza kazi balozi mdogo wa Uturuki mjini Jerusalem.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.