Pata taarifa kuu

Wapalestina tisa wameuawa katika shambulio la Israeli kwenye kambi ya wakimbizi

Nairobi – Wanajeshi wa Israeli wametekeleza mashambulio ya angani katika kambi ya wakimbizi ya Jenin, inayokaliwa na wakimbizi wa Palestina na kusababisha vifo vya watu tisa.

Shambulio hili linadaiwa kuwa mojawapo ya mashambulio makubwa zaidi kutekelezwa na wanajeshi wa Israeli katika Ukingo wa Magharibi
Shambulio hili linadaiwa kuwa mojawapo ya mashambulio makubwa zaidi kutekelezwa na wanajeshi wa Israeli katika Ukingo wa Magharibi AP - Nasser Nasser
Matangazo ya kibiashara

Hii ni operesheni kubwa ya kijeshi katika kambi hiyo ya Jenin ndani ya kipindi cha miaka 20.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema wanajeshi wake wanawalenga magaidi wanaojificha ndani ya kambi hiyo, wala sio wakimbizi wa Palestina.

Ripoti zinasema, wakimbizi Elfu tatu wamekimbia kutoka kwenye kambi hiyo, inayowapa hifadhi Wapalestina Elfu 18 baada ya kuanza kwa operesheni hiyo ya jeshi la Israeli.

Wizara ya Mambo ya nje ya Palestina, imelaani operesheni hiyo ya wanajeshi wa Israeli, ikisema Israeli inawalenga raia wa kawaida wa Palestina wanaoishi ndani ya kambi ya Jenin, madai ambayo hata hivyo Israeli imekanusha na kusema haifahamu ni lini operesheni hiyo itafika mwisho.

Mwaka 2002, jeshi la Israeli lilitekeleza shambulio lingine kwenye kambi hiyo na kusabisha vivo vya watu 52 na kusababaisha vifo vya wanajeshi 23, katika makabiliano ya siku 10.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.