Pata taarifa kuu

Jeshi la Israeli limeanza kuondoka kwenye kambi ya Jenin

Nairobi – Wanajeshi wa Israeli wameanza kujiondoa kwenye kambi ya Jenin inayokaliwa na Wapalestina katika eneo la ukingo wa Magharibi baada ya kutekeleza operesheni ya siku mbili, kuwasaka watu iliyosema ni magaidi, wanaotishia usalama wa Waisraeli.

Wanajeshi wa Israeli wamekuwa wakitekeleza oparesheni ya kijeshi katika kambi hiyo ya Jenin
Wanajeshi wa Israeli wamekuwa wakitekeleza oparesheni ya kijeshi katika kambi hiyo ya Jenin © AP/Majdi Mohammed
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu unamaliza operesheni hiyo ya kijeshi iliyosababisha vifo vya Wapalestina 12 na mwanajeshi mmoja wa Israeli.

Wakati wanajeshi wa Israeli wakianza kuondoka, kumesikika milio ya risasi na milipuko katika kambi hiyo, huku wakimbizi wa Palestina wakisherehekea kuondoka kwa vikosi hivyo.

Aidha, Israeli imesema imefanikiwa kuzuia maroketi matano yaliyorishwa Kusini mwa nchi yake na wanamgambo wa Kipalestina, katika ukanda wa Gaza, lakini hakuna kundi lililodai kuhusika.

Ripoti zaidi zinasema, mashambulio ya angaa yamelenga Kaskazini mwa Gaza asubuhi hii, lakini hakujaripotiwa kwa mauaji au majeruhi.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, alitangaza operesheni hiyo aliyosema ilikuwa inawasaka magaidi waliojficha ndani ya kambi hiyo, huku uongozi wa Palestina, ukiishtumu Israeli kwa kuwalenga raia wake wasiokuwa na hatia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.