Pata taarifa kuu

Afghanistan: Taliban 'wanalenga kuwafanya wanawake wasionekane', kulingana na UN

Vizuizi vilivyowekwa na Taliban kwa wanawake wa Afghanistan "vinalenga kuwafanya wanawake wasionekane" katika jamii,  mwandishi maalum wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu nchini Afghanistan, Richard Bennett amesema.

Wanawake wakivaa Burqa wakitembea karibu na askari wa Taliban katika moja ya mitaa ya Kabul Jumanne Mei 3.
Wanawake wakivaa Burqa wakitembea karibu na askari wa Taliban katika moja ya mitaa ya Kabul Jumanne Mei 3. © AP - Ebrahim Noroozi
Matangazo ya kibiashara

Tangu kurejea kwao madarakani Agosti mwaka jana, Taliban wameweka msururu wa vikwazo kwa jamii za watu, vingi vikilenga kuwatiisha wanawake kwenye dhana yao ya kimsingi ya Uislamu.

Kwa kiasi kikubwa wamezuiwa kuajiriwa katika mashirika ya umma, wamezuiwa haki yao ya kusafiri, na kuwazuia wasichana kwenda kaika shule za sekondari na za upili.

Mapema mwezi Mei, kiongozi mkuu wa Taliban alitoa agizo kwamba wanawake lazima wajisiutiri kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kufuniuka nyuso zao, hasa kwa vazi la burqa.

Hatua hizi zote "zinaelezea aiana fulani ya ubaguzi kamili wa kijinsia na zinalenga kuwafanya wanawake wasionekane katika jamii," Richard Bennett amesema katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu, mwishoni mwa ziara ya siku 11 nchini humo.

Mamlaka ya Taliban "ilishindwa kutambua ukubwa na uzito wa dhuluma zilizofanywa (kwa haki za binadamu), nyingi zikiwa katika jina lao", aliongeza.

Bw Bennett alifanya mkutano wake na wanahabari pindi tu Taliban waliokuwa na silaha walipovunja maandamano ya wanawake wakitaka shule za upili za wasichana zifunguliwe.

"Wanawake na wasichana wapatao 45 walikuwepo kwenye maandamano hayo, lakini vikosi vya Taliban vilivyojawa na hasira vilikuja na kututawanya," Munisa Mubariz, mratibu wa maandamano hayo, meliiambiashirika la habari la AFP.

Mnamo Machi 23, Taliban iliamuru kufungwa kwa shule zote za sekondari za wasichana, saa chache baada ya kufunguliwa kwa mara ya kwanza tangu vuguvugu hilo la wanamgambo wa Kiislamu kuchukua mamlaka.

Serikali hadi sasa haijatoa sababu za wazi za uamuzi huo wa kufungwa, lakini maafisa tangu wakati huo wamesema shule zitafunguliwa hivi karibuni, bila maelezo zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.