Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Mlipuko katika msikiti waua takriban watu 33

Takriban watu 33, wakiwemo watoto, wameuawa na wengine 43 kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea kwenye msikiti wa Sufi wakati wa sala ya Ijumaa kaskazini mwa Afghanistan, Taliban wamesema, siku moja baada ya mashambulizi mawili ya umwagaji damu yaliyodaiwa na kundi la Islamic State.

Wanajeshi wa Taliban na madaktari wanasubiri kuwasili kwa majeruhi nje ya hospitali baada ya shambulio lililosababisha vifo vya makumi ya watu kwenye msikiti wa Imam Sahib mkoani Kunduz.
Wanajeshi wa Taliban na madaktari wanasubiri kuwasili kwa majeruhi nje ya hospitali baada ya shambulio lililosababisha vifo vya makumi ya watu kwenye msikiti wa Imam Sahib mkoani Kunduz. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

"Mlipuko huo ulitokea katika msikiti wa Imam Sahib wilaya ya Kunduz, na kuua raia 33, wakiwemo watoto," msemaji wa serikali Zabihullah Mujahid amesema kwenye Twitter. Mmoja wahudumu wa afya wa hospitali iliyo karibu pia ameliambia shirika la habarila AFP kwamba kati ya watu 30 na 40 walikuwa wamelazwa katika hospitali hii baada ya mlipuko huu.

Tangu wapiganaji wa Taliban wachukue udhibiti wa Afghanistan mwezi Agosti baada ya kupindua mamlaka zinazoungwa mkono na Marekani nchini humo, idadi ya mashambulizi ya mabomu imepungua, lakini wanajihadi na IS wameendeleza mashambulizi yao dhidi ya malengo wanayoona kuwa ya uzushi. "Tunalaani uhalifu huu (...) na tunatoa pole kwa wafiwa," amesema Zabihullah Mujahid.

Makundi ya wanajihadi kama vile kundi la Islamic State wana chuki kubwa kwa dhehebu hili la Kiislamu ambalo wanaliona kuwa la uzushi na ambalo wanalituhumu kwa ushirikina - dhambi kubwa zaidi katika Uislamu - kwa kuomba uombezi wa watakatifu waliokufa.

Mlipuko huu unakuja siku moja baada ya mashambulizi mawili yaliyodaiwa na kundi la Islamic State nchini Afghanistan, ambapo kwa jumla yalisababisha vifo vya takriban watu 16 na wengine kadhaa kujeruhiwa. Waumini 12 walifariki dunia na 58 walijeruhiwa katika shambulio la Alhamisi dhidi ya msikiti wa Kisihia katika mji wa Mazar-i-Sharif (kaskazini). Siku hiyo, takriban watu wanne waliuawa na wengine 18 kujeruhiwa huko Kunduz wakati bomu lilipolipuka kwenye baiskeli huku gari lililokuwa limebeba mafundi wa kiraia wanaofanya kazi katika kitengo cha kijeshi cha Taliban likipita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.