Pata taarifa kuu

Afghanistan: Watangazaji wa TV waonekana nyuso zao zikiwa wazi

Nchini Afghanistan, watangazaji wa televisheni wa Afghanistan waliamua Jumamosi kukaidi amri ya Taliban inayowataka wanawake kufunika nyuso zao hadharani. Wengine walionekana kwenye televisheni wakiwa hafuniki nyuso zao, lakini Jumapili hii wamejirejea na kutekeleza amri.

Mtangazaji wa Zan TV,kituo cha televisheni kinachojitolea kwa wanawake, huko Kabul, Afghanistan. Picha hii  ya zamani ilipigwa Mei 30, 2017, hii ni kusema muda mrefu kabla ya Taliban uchukuwa madaraka Afghanistan.
Mtangazaji wa Zan TV,kituo cha televisheni kinachojitolea kwa wanawake, huko Kabul, Afghanistan. Picha hii ya zamani ilipigwa Mei 30, 2017, hii ni kusema muda mrefu kabla ya Taliban uchukuwa madaraka Afghanistan. © AP - Rahmat Gul
Matangazo ya kibiashara

Hii ni ishara ya kupinga baadhi ya sheria za utawala wa Taliban wakati tangu kuchukua madaraka mwezi Agosti 2021,Taliban wameweka mfululizo wa vikwazo vinavyoweka kikomo haki za wanawake. Huko Kabul, Arezo, ambaye jina lake tumelibadilisha kwa sababu za kiusalama, anafanya kazi katika kituo cha televisheni cha taifa, anaripoti mwandishi wetu, Sonia Ghezali. Amekataa hadi sasa kufunika uso wake. Lakini vita vyake vina mipaka.

Ikiwa tutaendelea kuvaa hijabu au kufunika nyuso zetu, basi labda watakamata familia zetu na labda tutapoteza kazi zetu. Na hilo haliendani na madai yetu, amebaini. Hatuna chaguo. Tunalazimika kufunika nyuso zetu. Hili ni tatizo la wanawake wote, si tu waandishi wa habari.

"Kila mtu anaogopa kupinga"

Magharibi mwa nchi, Fatima bado anatumai kuwa na uwezo wa kuwashawishi Taliban. "Kila mtu anaogopa kupinga," anasema. Lakini tutajaribu kukutana nao ili kuwaeleza kuwa namna yetu ya kuvaa hijabu ni ya Kiislamu na tutajaribu kupigania haki zetu. Lakini wakikataa kutusikiliza, ni lazima tutii. »

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.