Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Watu kumi wafariki katika mlipuko dhidi ya msikiti wa Sunni Kabul

Takriban watu kumi waliuawa katika mlipuko uliotokea katika msikiti wa Sunni mjini Kabul siku ya Ijumaa baada ya swala ya Ijumaa, huku Afghanistan ikikabiliwa na mashambulizi ya kukithiri mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Waafghanistan wanazurura katika kitongoji cha Serahi Alauddin huko Kabul baada ya mlipuko kwenye msikiti siku ya Ijumaa (tarehe 29 Aprili).
Waafghanistan wanazurura katika kitongoji cha Serahi Alauddin huko Kabul baada ya mlipuko kwenye msikiti siku ya Ijumaa (tarehe 29 Aprili). REUTERS - ALI KHARA
Matangazo ya kibiashara

Walengwa wa shambulio hilo wanaonekana kuwa watu wa jamii ya Wasufi walio wachache wanaofanya tambiko baada ya sala ya Ijumaa, afisa mmoja alisema.

Vikundi vya kijihadi kama vile Islamic State vina chuki kubwa kwa dhehebu hili la Kiislamu ambalo wanaliona kuwa la uzushi.

Waathiriwa walisafirishwa kwa magari ya wagonjwa mahututi na magari ya kawaida hadi hospitali katikati mwa Kabul, lakini Taliban waliwazuia waandishi wa habari kuingia katika kituo hicho.

Makundi ya wanawake yalikuwa yakilia nje ya hospitali na karibu na msikiti katika kujaribu kutafuta wapendwa wao, mwandishi wa shirika la habari la AFP alibainisha.

"Takriban watu 300 hadi 400 walikuwa wakifanya matambiko wakati mlipuko huo ulipotokea," mkazi wa eneo hilo.

"Nilisaidia usafiri watu 10 hadi 15 waliojeruhiwa na watu watatu waliouawa. Wengi waliojeruhiwa na wahanga bado wanahamishwa."

"Waumini wengi walikuwa msikitini (...) wakati mlipuko ulipotokea. Waathiriwa kadhaa waliangushwa (na mlipuko huo)," mtu aliyenusurika, ambaye alisema jina lake ni Ahmad, aliliambia shirika la habari la AFP.

Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, Ramiz Alakbarov, amelaani shambulio hilo. "Shambulio la leo (...) ni pigo jingine kwa watu wa Afghanistan ambao wanaendelea kukabiliwa na ukosefu wa usalama na ghasia zisizoisha," alisema katika taarifa yake.

Msururu wa mashambulio mabaya ya mabomu, ambayo baadhi yanadaiwa na kundi la Islamic State (IS), yamesababisha makumi ya vifo nchini humo katika muda wa wiki mbili zilizopita.

Mlipuko huo unakuja saa chache baada ya ujumbe kutoka kwa kiongozi mkuu wa nchi hiyo, Hibatullah Akhundzada, kutangazwa kabla ya Eid al-Fitr, "sikukuu ya kufuturu" ambayo inaashiria kumalizika kwa Ramadhani.

Hakutaja mashambulizi ya hivi majuzi, akifurahi tu kwamba Afghanistan iliweza kuunda "jeshi lenye nguvu la Kiislamu na la kitaifa", pamoja na "huduma thabiti ya kijasusi".

Usalama ulikuwa umeimarishwa sana nchini Afghanistan baada ya Taliban kurejea madarakani mwezi Agosti, ingawa Dola la Kiislamu-Khorasan (ISIS-K), tawi la ISIS katika eneo hilo, liliendelea kufanya mashambulizi mabaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.