Pata taarifa kuu
MAREKANI-USHIRIKIANO

Washington kutuma meli na ndege za kivita UAE dhidi ya waasi Houthi

Marekani wiki hii imetangaza kuwa iko tayari kutuma meli ya kivita na ndege za kivita kusaidia Umoja wa Falme za Kiarabu dhidi ya waasi wa Houthi katika kukabiliana na ongezeko la mashambulizi ya waasi hao wa Yemen dhidi ya nchi hiyo ya Ghuba, ambako wanajeshi wa Marekani wamepiga kambi.

Abou Dhabi, mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu.
Abou Dhabi, mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu. Flickr/Joi Ito
Matangazo ya kibiashara

Kutumwa huku, tarehe ambayo haijabainishwa na ambayo lazima "isaidie Umoja wa Falme za Kiarabu kukabiliana na tishio la sasa", inafuatia mazungumzo ya simu siku ya Jumanne kati ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, na mwanamfalme wa Abu Dhabi na Mtawala wa nchi hiyo, Mohammed bin Zayed al-Nahyan, Ubalozi wa Marekani nchini Umoja wa Falme za Kiarabu umesema katika taarifa yake. Washington inapanga vikosi vya kijeshi katika eneo ambalo jeshi la Marekani tayari linapiga kambi, ikiwa na kambi za jeshi nchini Qatar, Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Umoja wa Falme za Kiarabu ni sehemu ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia, ambayo tangu mwaka 2015 imekuwa ikisaidia serikali ya Yemen katika vita dhidi ya Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran. Mnamo mwezi Januari, Umoja wa Falme za Kiarabu ulilengwa na mashambulizi matatu ya waasi wa Houthi.

Tarehe 17, shambulio la ndege isiyo na rubani na kombora dhidi ya mitambo ya mafuta na uwanja wa ndege wa Abu Dhabi liliua watu watatu. Mnamo tarehe 24, makombora mawili ya masafa marefu yaliyolenga kituo cha anga cha Al-Dhafra, ambapo vikosi vya Marekani vinapiga kambi, yaliharibiwa na wanajeshi hao.

Shambulio la hivi punde, lililotokea Jumatatu Januari 31, liliambatana na ziara rasmi ya kwanza ya Rais wa Israel Isaac Herzog katika Umoja wa Falme za Kiarabu tangu nchi hizo mbili zifufue uhusiano wao mwaka wa 2020.

Chombo cha kuangamiza kombora cha USS Cole kitashirikiana na Jeshi la Wanamaji la Imarati na kitaegesha huko Abu Dhabi, mji mkuu wa Imirati, kulingana na taarifa hiyo, ambayo ilisema Washington pia itapeleka ndege za kivita za kizazi cha tano. Msaada huu ni "ishara ya wazi kwamba Marekani inaunga mkono Umoja wa Falme za Kiarabu, mshirika wa kimkakati wa muda mrefu", taarifa hiyo imeongeza.

Aidha, Marekani itaendelea kutoa taarifa za kijasusi kwa ajili ya kuzuia mashambulizi, kulingana na taarifa hiyo. Kuongezeka kwa mashambulizi ya Houthi dhidi ya Umoja wa Falme za Kiarabu, nchi tajiri ya Ghuba ambayo inashikilia sifa yake kama kisima cha amani katika Mashariki ya Kati, inaashiria hatua mpya katika vita vya Yemen vilivyoanza mnamo 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.