Pata taarifa kuu

Marekani: Joe Biden akaribisha mkataba wa amani kati ya Israel na UAE

Hatua ya kufufua uhusiano kati ya Umoja Falme za Kiarabu na Israeli iliyotangazwa Alhamisi wiki hii na Donald Trump inatoa ushindi muhimu wa kidiplomasia kwa rais huyo wa Marekani, ikisalia miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa urais.

Joe Biden huko Wilmington, katika Jimbo la Delaware, Agosti 12, 2020.
Joe Biden huko Wilmington, katika Jimbo la Delaware, Agosti 12, 2020. AP Photo/Carolyn Kaster
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya White Haouse imeendelea kusisitiza jukumu lake katika mkataba huo. Hata mgombea urais kutoka chama cha Democratic, Joe Biden, amekaribisha mkataba huo wa amani.

Huu mkataba wa kihistoria," amekiri Joe Biden. Lakini katika taarifa yake, mgombea huyu wa chama cha Democratic amejizuia kutaja jina la Donald Trump. Joe Biden anadai kwamba hatua ya kufufua uhusiano kati ya Israeli na Umoja wa Falme za Kiarabu ni juhudi za serikali kadhaa za Marekani, ikiwa ni pamoja na ile ya Barack Obama.

Hata hivyo Donald Trump analinganisha tukio na mkataba wa amani wa kihistoria kati ya Misri na Israeli uliotiliwa saini baada ya upatanishi wa Marekani.

"Hii ni habari kubwa mno. Ulimwengu wote unaizungumzia, ulimwengu wote, ni jambo la kushangaza: tumekamilisha mkataba wa amani wa kihistoria kati ya Israeli na Umoja wa Falme za Kiarabu, Rais wa Marekani amesema. Baada ya nusu karne Israeli na Falme za Kiarabu wameamua kufufua uhusiano wao wa kidiplomasia. Hakuna mtu aliyefikiria kuwa hili linaweza kutokea. Ni mafanikio makubwa tangu kutiliwa saini mkataba wa amani wa kihistoria kati ya Israeli na Misri, zaidi ya miaka arobaini iliyopita, " amebaini rais wa Marekani donald Trump.

Kwa mujibu wa rais wa Marekani, zoezi la kutia saini kwenye mkataba huo litafanyika katika Ikulu ya White ndani ya wiki tatu zijazo.

Donald Trump amehakikisha kwamba nchi zingine za Kiarabu zitafuata mfano wa Umja wa Falme za Kiarabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.