Pata taarifa kuu
MAREKANI-BIDEN-HARRIS-SIASA-AFYA

Joe Biden na Kamala Harris watoa wito kwa Wamarekani kuvaa barakoa kudhibiti Corona

Mgombea urais kupitia chama che Democratic nchini Marekani Joe Biden na mgombea mwenza wake Kamala Harris, sasa wanataka uvaaji wa barakoa liwe suala la kitaifa na kizalendo katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

Kamala Harris akiambanata na Joe Biden, katika kampeni ya uchaguzi wa uraisa huko Wilmington katika Jimbo la Delaware, Agosti 12, 2020.
Kamala Harris akiambanata na Joe Biden, katika kampeni ya uchaguzi wa uraisa huko Wilmington katika Jimbo la Delaware, Agosti 12, 2020. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao wakizungumwa wakiwa wamevalia barakoa, Biden ambaye ameendelea kumkosoa rais Donald Trump kuhusu namna alivyoshughulikia janaga hili, ametaka uuvaji wa barakoa uwe ni lazima kwa muda wa miezi mitatu ijayo.

“Kila Mmarekani avalie barakoa akiwa nje ya nyumbani kwake kwa muda wa miezi mitatu ijayo. Kila Gavana lazima ahakikishe kuwa uvaaji wa barakoa unakuwa lazima kwa sababu watalaam wanasema kuwa itasaidia kuokoa maisha ya watu zaidi ya Elfu 40 kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo. Kuwa mzalendo ili kuokoa maisha ya Wamerekani, “ amebaini Joe Biden..

Kauli hii imeungwa mkono na mgombea mwenza wake Bi Harris.

“Huu ndio uongozi wa kweli. Na Wamarekani wanamfahamu Joe na namba yake ya kuongoza nchi, siku zote atafanya kilicho bora kwa ajili ya watu na nchi hii, “ amesema Seneta Kamala Harris .

Nae rais Donald Trump, akizungumzia suala hili, amesema anaamini kuwa, maambukizi hayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya Laki Moja na Elfu Sitini nchini humo yatakwisha.

Haya yanajiri wakati maafisa wa ujasusi nchini Marekani wanaamini Urusi inaendesha njama dhidi ya mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden, huku washirika wa Kremlin wakifanyakazi kuimarisha kampeni ya Trump.

Mkuu wa kitengo cha kupambana na ujasusi wa nje nchini Marekani William Evanina, amesema maafisa wa ujasusi wanaamini pia kwamba China haitaki Trump ashinde muhula wa pili na imeongeza ukosoaji wake wa ikulu wa White House, ikipanua juhudi zake za kushawishi sera ya umma nchini Marekani, ili kuwawekea shinikizo wanasiasa wanaoonekana kuwa wapinzani wa maslahi ya China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.