Pata taarifa kuu
ISRAEL-DIPLOMASIA

Israel haina mpango wa kuziuzia nchi za Kiarabu kifaa chake cha kuzuia makombora

Makubaliano ya Abraham, makubaliano haya ya kurekebisha uhusiano kati ya Israeli na baadhi ya nchi za Kiarabu, "yamefanywa ili yaweze kudumu", ametangaza Rais wa Israel, Isaac Herzog, ambaye kwa sasa yuko katika ziara rasmi katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Usafirishahi wa kifaa cha kuzuia kombora katika eneo la Ashdod, Novemba 17, 2012.
Usafirishahi wa kifaa cha kuzuia kombora katika eneo la Ashdod, Novemba 17, 2012. REUTERS/Darren Whiteside
Matangazo ya kibiashara

Ziara yake ilitatizwa na makombora ya masafa marefu, yaliyorushwa na waasi wa Houthi kutoka Yemen, dhidi ya Abu Dhabi. Kulingana na vyombo kadhaa vya habari vya Israel, Umoja wa Falme za Kiarabu ilijaribu kupata "Iron Dome", kifaa cha Israeli cha kuzuia makombora. Lakini serikali ya Israel haiko tayari kutoa ujuzi wake.

Linapokuja suala la teknolojia ya kisasa ya kijeshi, urafiki wa Israel na Imarati unaonekana kuwa na kikomo, vyombo vya habari kadhaa vya Israel vinaripoti.

Mkataba wa Abraham au la, Israel kamwe haiwezi kuuza kifaa chake cha kuzuia makombora kwa nchi za Kiarabu, ambazo ndiyo kwanza imetiliana saini mikataba ya amani, Alon Ben David, mchambuzi wa kijeshi wa Israel, ameelezea maikitiko yake katika gazeti la kila siku la Maariv.

Kulingana mchambuzi huyo, Israel ingelikosa fursa ya kutia saini mkataba wa dola bilioni tatu na nusu.

Mgawanyiko ndani ya idara za usalama za Israel

Waziri Mkuu wa Israel Naftali Bennett amejaribu kuonyesha ushahidi wa diplomasia. Kulingana na vyombo vya habari vya Israel, amejaribu kumtuliza mwana mfalme wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mohammed bin Zayed, kwa kudai kufanya kazi ili kuipa Abu Dhabi "msaada unaohitajika".

Lakini kulinganana duru za kuaminika, idara za usalama za Israeli zinasemekana kugawanyika katika suala hilo. Idara ya ujasusi ya Israel, Mossad, linaunga mkono hilo, lakini sio jeshi, ambalo linahofia kwamba "teknolojia yake au ujuzi wake unaweza kuapitishwa kwa nchi ningine".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.