Pata taarifa kuu
ISRAEL-ULINZI

Israel yakamilisha ujenzi wa kizuizi kinachoitenga na Gaza

Wakati eneo hilo limeishi chini ya vizuizi maradufu vya Israel na Misri tangu mwaka 2007 na kundi la Kiislamu la Palestina Hamas kutwaa madaraka, eneo hili la Palestina lenye wakaazi milioni mbili limezingirwa kwa miaka kadhaa. Israel ilichukua zaidi ya miaka mitatu kukamilisha uzio huu wa usalama, uliotajwa kuwa kazi bora ya kiteknolojia.

Wanajeshi wa Israel wakipiga doria kwenye sherehe ya kukamilisha ujenzi wa kizuizi kipya kinachoitenganisha nchi hiyo na Ukanda wa Gaza, Desemba 7, 2021.
Wanajeshi wa Israel wakipiga doria kwenye sherehe ya kukamilisha ujenzi wa kizuizi kipya kinachoitenganisha nchi hiyo na Ukanda wa Gaza, Desemba 7, 2021. AP - Tsafrir Abayov
Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa Israel ilikuwa na uzio, kifaa cha kuzuia makombora, ili kujikinga na kitendo cha urushwaji roketi na makundi ya Wapalestina yenye silaha kutoka Gaza. Lakini Israel sasa ina "ukuta wa chuma".

Kizuizi cha kilomita 65, kilicho na mamia ya kamera, vitambuzi, rada, au tani 140,000 za chuma. Pia ina sehemu ya chini ya ardhi. Lengo, kulingana na jeshi la Israeli: kuzuia kupenya kwa wanajeshi wa Hamas na kuingia katika ardhi ya Israeli kupitia mifereji ya maji huko Gaza.

Kizuizi hiki kipya kiligharimu zaidi ya dola bilioni 1. Kinaenea hadi baharini na pia kimeunganishwa na mfumo wa silaha unaodhibitiwa kwa mbali.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000, Israeli pia ilizindua ujenzi wa ukuta wa kutenganisha na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa. Urefu wa kilomita 700, sehemu zingine zimetengenezwa kwa simiti iliyoimarishwa na kupanda hadi mita nane juu. Kizuizi hiki, ambacho bado kinaendelea kukamilika, kimepewa jina la "ukuta wa ubaguzi wa rangi" na Wapalestina na baadhi ya mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.