Pata taarifa kuu
ISRAEL-USALAMA

Israeli yatangaza mashirika sita kutoka Palestina kuwa ya "kigaidi"

Mashirika sita yasio ya kiserikali kutoka Palestina yamewekwa kwenye orodha ya "mashirika ya kigaidi" na serikali ya Israeli. Kulingana na Wizara ya Ulinzi, wamehusishwa na Chama cha Wananchi kwa Ukombozi wa Palestina PFLP.

Wizara ya Ulinzi ya Israeli imetangaza mashirika sita yasio ya kiserikali kutoka Palestina kuwa ni ya kigaidi. Hapa, ni Benny Gantz, Waziri wa Ulinzi.
Wizara ya Ulinzi ya Israeli imetangaza mashirika sita yasio ya kiserikali kutoka Palestina kuwa ni ya kigaidi. Hapa, ni Benny Gantz, Waziri wa Ulinzi. AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa miaka mingi PFLP, kundi lenye silaha la Palestina, limekuwa ikichukuliwa kama kundi la kigaidi na serikali ya Israel, lakini pia na Umoja wa Ulaya. Mashirika kadhaa ya haki za binadamu, ya kimataifa, na hata ya kutoka nchini Israeli, yamekosoa uamuzi huu.

Kwa kuyataja mashirika haya sita kutoka Palestina kuwa ni ya kigaidi, Israeli inajipa haki ya kukomesha shughuli zao. Chini ya sheria ya serikali ya Israel, mamlaka nchini humo sasa itaweza kufunga ofisi zao, kuzuia mali zao, na kuwakamata na kuwafunga wajumbe na wafanyakazi wa mashirika hayo.

Kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Ulinzi ya Israeli, idara za ujasusi za ndani nchini Israel imejumuisha mashirika hayo sita na Chama cha Wananchi kwa Ukombozi wa Palestina.

Ufadhili wa "shughuli za kigaidi" za PFLP

"Chini ya kisingizio cha shughuli za kiraia […] mashirika haya yananufaika na misaada kutoka mataifa ya Ulaya kwa njia haramu," imesema taarifa hiyo. Fedha hizi ziliruhusu chama cha PFLP kufadhili familia za wafungwa [Wapalestina nchini Israel], wahusika wa mashambulizi, kulipa mishahara kwa wanachama wake, kuimarisha shughuli zake za kigaidi na kueneza itikadi yake. "

Madai hayo yamekanushwa mara moja na mashirika ya haki za binadamu. Shirika lisilo la kiserikali lnchini Israel la B'Tselem linalaani vikali uamuzi huu, na limeitaja serikali ya Israel kuwa ni "utawala wa kibaguzi, wa kiimla na wenye vurugu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.