Pata taarifa kuu
ISRAEL-HAKI

Israeli: Wafungwa wawili wakipalestina kati ya sita waliotoroka wakamatwa

Wawili kati ya wafungwa sitawa Kipalestina waliotoroka hivi karibuni jela lenye ulinzi mkali wanashikiliwa na idara za usalama baada ya kukamatwa Ijumaa jioni wiki hii. Kutoroka kwao kulidumu siku chache.

"Kundi la Islamic Jihad, mashujaa waliotoroka kutoka gereza la Gilboa," ni maneneo yaliyoandikwa kwenye bango ambalo linaonyesha picha za wafungwa sita wa Kipalestina waliotoroka kutoka gereza la Israeli katika kambi ya wakimbizi ya Jenin, katika Ukingo wa Magharibi, Septemba 8, 2021.
"Kundi la Islamic Jihad, mashujaa waliotoroka kutoka gereza la Gilboa," ni maneneo yaliyoandikwa kwenye bango ambalo linaonyesha picha za wafungwa sita wa Kipalestina waliotoroka kutoka gereza la Israeli katika kambi ya wakimbizi ya Jenin, katika Ukingo wa Magharibi, Septemba 8, 2021. AP - Nasser Nasser
Matangazo ya kibiashara

Chini ya wiki moja baada ya wafungwa sita wa Kipalestina kutoroka gereza la Israeli, tukio lililowashangaza wengi, wawili kati yao walikamatwa Ijumaa jioni. Msako huo unaendelea katika jaribio la kuwapata wengine waliotoroka.

Mohamed Ardha na Yacoub Qadri, wawili kati ya wafunwa hao sita, walikamatwa huko Nazareth, mji unaokaliwa na watu wengi kutoka jamii ya Waarabu Kiisrael karibu kilomita thelathini kutoka jela lenye ulinzi mkali walikokuwa wakizuiliwa. Katika picha zilizorushwa na televisheni ya Israeli, wafungwa hao walionekana nyuso zao zikifunikwa.

Familia ya Yacoub Qadri inasema ina huzuni lakini wamefarijika, aamesema mpwa wake Mahmoud Qadri. "wangelikamatwa tu, kwani hawabnesalia mafichoni maisha yao yote. Mjomba wangu anatumikia kifungo cha maisha, afadhali aliona mwanga wa jua kwasiku chache nakufurahia uhuru wa wiki moja. Na tunasema, "Kwa bahati nzuri bado yuko hai." "

Tangu kutoroka kwa wafungwa hao mapema wiki hii, familia za zao zilifufia kuwa watapigwa risasi katika msako uliozinduliwa na vikosi vya Israeli. Polisi na Jeshi wapeleka silaha za kivita kuwapata wafungwa hao sita waliotoroka kupitia handaki lililochimbwa chini ya gereza walikokuwa wanazuiliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.