Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA

Gaza: Human Rights Watch yalaani "uhalifu wa kivita"

Shirika la kimataifa la Haki za binadamu la Human Rights Watch limebaini katika ripoti yake mpya kwamba makabiliano kati ya wanamgambo wa Hamas na jeshi la Israel yalisababisha vifo vya Wapalestina 260, ikiwa ni pamoja na watoto 66. Kwa upande wa Israel watu 13 waliuawa, ikiwa ni pamoja na watoto wawili.

Mashambulizi ya Israeli huko Gaza, Mei 13, 2021.
Mashambulizi ya Israeli huko Gaza, Mei 13, 2021. AP - Hatem Moussa
Matangazo ya kibiashara

Human Rights Watch inasema jeshi la Israeli na makundi yenye silaha ya Wapalestina wamevunja sheria za vita, wakishambulia raia kwa makusudi.

Human Rights Watch imetathimini mashambulizi matatu ya anga ya jeshi la Israel: lile la Mei 10 huko Beit Hanoun kaskazini mwa ukanda huo, lile la Mei 15 katika kambi ya wakimbizi ya al-Shati, na shambulio lingine lililotekelezwa katika mtaa wa Al-Wehda katikati ya Jiji la Gaza. Kwa mashambulio yote hayo, Wapalestina 62 waliwaua.

Baada ya kufanya mahojiano zaidi ya thelethini, uchunguzi kwenye maeneo ya  matukio na wakaazi na katika maeneo yaliyolengwa, shirika hilo la haki za binadamu limebaini: "Vikosi vya Israeli viliangamiza familia nyingi, wakati hakuna kambi wata kituo cha jeshi kilichokuwa karibu na maeneo hayo yenye makaazi. "

Ripoti hiyo pia inazungumzia msimamo wa Israel kukataa mara kwa mara kufanyika kwa uchunguzi wa madai ya uhalifu wa kivita, ama kwa kuzuia kuingia kwa watafiti huko Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.