Pata taarifa kuu

Israeli-Palestina: Bennett na al-Sisi wakutana kufufua mchakato wa amani

Waziri Mkuu wa Israel Naftali Bennet alifanya ziara ya kiserikali nchini Misri Jumatatu, Septemba 13. Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa serikali ya Israeli kutzuru nchi hiyo tangu mwaka 2011. Alikutana na rais Abdel Fattah al-Sisi huko Sharm el-Sheikh. Wawili hao walizzungumzia hasa juu ya kuzinduliwa tena kwa mchakato wa amani kati ya Palestina na serikali ya Kiyahudi, ambao umekwama tangu 2014.

Waziri Mkuu wa Israeli Naftali Bennett (kushoto) na rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi (kulia), Septemba 13, 2021 huko Sharm el-Sheikh.
Waziri Mkuu wa Israeli Naftali Bennett (kushoto) na rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi (kulia), Septemba 13, 2021 huko Sharm el-Sheikh. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa Israeli alipokelewa Misri, hii haikutokea kwa zaidi ya miaka kumi, amebaini mwandishi wetu huko Jerusalem Sami Boukhelifa. Tangu Januari 2011, Benjamin Netanyahu alifanya ziara nchi Misri, wakati nchi hiyo ilikuwa bado ikitawaliwa na Hosni Mubarak. Siku chache baadaye, raïsalitimuliwa mamlakani kufuatia maandamano ya raia yaliyozukakatika nchi nyingi za Kiarabu.

Muongo mmoja umepita, kipindi ambacho uhusiano kati ya nchi hizi mbili ulionekana kuimarika na kuzorota. Lakini mwishowe, miaka michache iliyopita kuliripotiwa ushirikiano wa karibu wa usalama, na hasa vita dhidi ya makundi ya kigaidi huko Sinai. Nchi hizo mbili pia zimeshirikiana katika mpango wa nishati: tangu 2020, Israel husafirisha gesi yake kwenda Misri.

Misri, ambayo pia inafanya mazungumzo na maafisa wa Mamlaka ya Palestina na wale walio madarakani na Hamas huko Gaza, inatafuta kufufua mazungumzo ya amani kati ya Israeli na Palestina. Mpango huu tayari ulikuwa umejadiliwa katika mkutano wa kilele mnamo mwezi Agosti na mkuu wa Mamlaka ya Palestina na Mfalme wa Jordaan. Israel, kwa upande wake, imewasilisha tu mpango wa kukarabati Gaza, kwa sharti kwamba Hamas itaepukana na "machafuko." Na Israeli inahitaji msaada wa Misri kufikia lengo lake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.