Pata taarifa kuu

Mashariki ya Kati: Mvutano waibuka kati ya Israeli na Gaza

Kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya Israel na Gaza baada ya majibizano ya risasi Jumatano ya wiki iliyopita katika pande zote za mpaka, kisha maroketi na moja ya mashambulizi ya kijeshi ya anga ya Israel. Yote haya yanakuja baada ya wiki kadhaa za utulivu.

"Wale wanaoelekeza roketi kwa Israel lazima wawajibike kikamilifu," Waziri Mkuu wa Israel Naftali Bennett ametangaza Jumapili (Januari 2) baada ya jeshi la Israel kurushiana risasi na Gaza.
"Wale wanaoelekeza roketi kwa Israel lazima wawajibike kikamilifu," Waziri Mkuu wa Israel Naftali Bennett ametangaza Jumapili (Januari 2) baada ya jeshi la Israel kurushiana risasi na Gaza. NIR ELIAS POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel yalilenga maeneo ya Hamas na pia eneo la kutengeneza roketi. Kwa mara ya kwanza kabisa, helikopta za Israeli zilishambulia kwa makombora ya Sam-7, makombora yanayobebeka kutoka ardhini hadi angani pia yanayojulikana kama Strela-2. Vifaa hivyo havikufikia malengo , chanzo cha jeshi la Israeli kimesema.

Shambulio hilo la anga la Israel linafuatia roketi mbili zilizorushwa jana asubuhi, Jumamosi, kutoka eneo la Palestina. ZIlianguka baharini karibu na pwani ya Tel Aviv. Tarehe 1 Januari ilikuwa kumbukumbu ya kuanzishwa kwa chama cha Fatah, tarehe inayoelezea mashambulizi haya mawili yanayohusishwa kundi hili la wanahad wa Kiislamu.

Hamas kwa upande wake inadai kwamba makombora hayo mawili yalirushwa kwa bahati mbaya kutokana na hali mbaya ya hewa. Maelezo mengine ni kwamba ni onyo linalohusishwa na mgomo wa njaa wa siku 137 wa mwanaharakati wa Kipalestina Hisham Abu Hawash anayezuiliwa nchini Israel.

Hoja nyingi sana ambazo zinakataliwa moja kwa moja na Israeli. Wale wanaoelekezea Israel maroketi lazima wawajibike kikamilifu, amesema Waziri Mkuu wa Israel Naftali Bennett.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.