Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Mji mkuu wa yemen, Sana'a, wakumbwa na mashambulizi baada ya UAE kushambuliwa

Muungano unaopambana dhidi ya waasi wa Kihouthi ulitangaza Jumatatu jioni, Januari 17, kufanya mashambulizi ya anga mjini Sanaa, mji mkuu unaodhibitiwa na waasi wa Yemen, baada ya shambulio baya huko Abu Dhabi lililodaiwa na Wahouthi, ikiwa ni shambulio la kwanza katika ardhi ya Umoja wa Falme za Kiarabu.

Maghala ya kuhifadhia mafuta ya Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Abu Dhabi (ADNOC) katika mji mkuu wa Falme za Kiarabu Abu Dhabi? Januari 17, 2022. Malori matatu ya lori yalilipuka karibu na eneo hilo siku ya Jumatatu na kuua watu watatu.
Maghala ya kuhifadhia mafuta ya Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Abu Dhabi (ADNOC) katika mji mkuu wa Falme za Kiarabu Abu Dhabi? Januari 17, 2022. Malori matatu ya lori yalilipuka karibu na eneo hilo siku ya Jumatatu na kuua watu watatu. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Muungano unaopambana dhidi ya waasi nchini Yemen ulitangaza Jumatatu jioni kuvamia Sanaa, mji mkuu unaodhibitiwa na waasi wa Kihouthi, baada ya shambulio baya katika Umoja wa Falme za Kiarabu, mwanachama wa muungano huu wa kijeshi. "Katika kukabiliana na tishio na hitaji la kijeshi, mashambulizi ya anga yanaanza mjini Sanaa," shirika la habari la serikali ya Saudi Arabia (SPA), ambalo linaongoza muungano huu limetangaza kwenye ukurasa wake wa Twitter.

"Ndege ya kivita ya F-15 pia iliharibu mitambo miwili ya kurusha makombora ya masafa marefu ambayo ilitumika siku ya Jumatatu," amesema msemaji wa muungano huo, Jenerali Turki Al-Maliki, kutoka Saudi Arabia. Mashambulizi hayo pia yanaripotiwa kuwalenga viongozi kadhaa wa Kihouthi kaskazini mwa mji mkuu wa Yemen. Vifo kadhaa vimeripotiwa kulingana na kituo cha televisheni cha Al Masirah TV chenye ushirikiano na aasi wa Houthi, ameripoti mwandishi wetu katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Nicolas Keraudren.

Mashambulizi haya ya anga yanafuatia mlipuko wa lori tatu za mafuta katika eneo la viwanda la Abu Dhabi karibu na maghala ya kuhifadhia mafuta ya Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Abu Dhabi (ADNOC)) na mlipuko mwingine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi. Mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya Mpakistani mmoja na Wahindi wawili, limebaini shirika la habari la serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu, WAM, ambalo pia limeripoti "watu sita waliojeruhiwa". "Moto mdogo" pia uliripotiwa katika eneo la ujenzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa jiji hilo.

Milipuko hii, ambayo kwa mara ya kwanza ilielezewa na mamlaka ya Imarati kama "ajali" iliyosababishwa na "vitu vidogo vinavyoruka, labda ndege zisizo kuwa na rubani", ilidaiwa na waasi wa Yemen. "Vikosi vya kijeshi (vya Houthis) vilifanya operesheni ya kijeshi yenye ubora na yenye mafanikio ndani ya mfumo wa operesheni iliyopewa jina la Kimbunga cha Yemen," alihakikisha msemaji wao, Yahya Saree, katika taarifa iliyorushwa kwenye kituo cha habari cha Al-Massira. "Maeneo mengi muhimu na ya kimkakati ya Imarati na vifaa" vililengwa kwa makombora ya masafa marefu na ndege zisizo kuwa na rubani, alisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.