Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Yemen: Kufungwa kwa uwanja wa ndege wa Sana'a kunazuia shughuli za kibinadamu

Uwanja wa ndege wa Sana'a, ulio mikononi mwa waasi wa Houthi, umefungwa kwa ndege za mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu na za Umoja wa Mataifa tangu Jumanne. Hatua hiyo imekuchukuliwa kutoaka na mashambulizi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia.

Majengo ya uwanja wa ndege wa Sana'a yaliharibiwa na mashambulizi ya anga ya muungano unaoongozwa na Suadi Arabia Desemba 21, 2021.
Majengo ya uwanja wa ndege wa Sana'a yaliharibiwa na mashambulizi ya anga ya muungano unaoongozwa na Suadi Arabia Desemba 21, 2021. REUTERS - KHALED ABDULLAH
Matangazo ya kibiashara

Riyadh inasema imejibu mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za waasi wa Houthi. Lakini hatu hiyo inaathiri mashirika yasiyo ya kiserikali na kwa kwa raia wanaoishi kwa msaada wa kibinadamu.

Baada ya mashambulizi ya muungano huo, uwanja wa ndege katika mji mkuu wa Yemen haujapokea tena ndege za Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa ya kutoa msaada wa kiutu kibinadamu tangu Jumanne wiki hii.

Siku ya Jumatatu jioni, muungano huo ulidai kuwa ulifanya "mashambulizi makubwa ya anga yaliyolenga maeneo ya kijeshi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sana'a". Operesheni "iliyofanywa kukabiliana na tishio na matumizi ya miundombinu ya viwanja vya ndege kuanzisha mashambulizi ya kuvuka mpaka," muungano huo umesema katika taarifa, ukinukuliwa na shirika la habari la serikali ya Saudi Arabia la SPA. Vikosi vya muungano vililenga maeneo sita katika uwanja wa ndege, ikijumuisha maeneo yanayokusudiwa "kutekeleza mashambulizi ya mabomu ya ndege zisizo na rubani" na "kufundisha magaidi" kwa kutumia vyombo hivi, muungano umeongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.