Pata taarifa kuu

Vita Yemen vyazua sintofahamu kati ya Saudi Arabia na Lebanon

Saudi Arabia imemrejesha nyumbani balozi wake nchini Lebanon na kumtaka balozi wa Lebanon kuondoka nchini humo ndani ya kipindi cha saa 48 baada ya taarifa ya Waziri wa Habari wa Lebanon kukosoa uingiliaji kati wa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Riyadh nchini Yemen, taarifa imebaini.

Wapiganaji watiifu kwa serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia karibu na uwanja wa vita huko al-Jawba, katika jimbo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo la Marib mnamo Oktoba 27, 2021.
Wapiganaji watiifu kwa serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia karibu na uwanja wa vita huko al-Jawba, katika jimbo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo la Marib mnamo Oktoba 27, 2021. - AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imesema kwamba Riyadh imeamua "kumrejesha nyumbani balozi wake nchini Lebanon kwa mashauriano, imemtaka balozi wa Lebanon katika nchini humo kuondoka katika nci hiyo ndani ya kipindi cha saa 48 na kuamua kusimamisha uagizaji wa vifaa vyovyote kutoka Lebanon".

Muungano wa kimataifa unaoongozwa na Saudi Arabia unazidisha mashambulizi dhidi ya waasi wa Houthi katika eneo la kimkakati la Marib mashariki mwa Yemen.Wiki hii msemaji wa waasi alitoa wito wa kuendelea na mapigano.

Mapigano kati ya vikosi vya serikali vinavyosaidiwa na mungano wa Kirabu unaoongozwa na Saudi Arabia na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran yamekithiri karibu na mji wa Marib, ulioko katika mkoa ambao rasilimali nyingi za hydrocarbon nchini hupatikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.