Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Yemen: Waasi wasiopungua 260 wauawa kwa kipindi cha siku tatu karibu na Marib

Muungano wa kimataifa unaoongozwa na Saudi Arabia unazidisha mashambulizi dhidi ya waasi wa Houthi katika eneo la kimkakati la Marib mashariki mwa Yemen. Msemaji wa waasi ametoa wito wa kuendelea na mapigano.

Mpiganaji anayeunga mkono serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia akikabiliana na waasi wa Houthi katika mkoa wa Marib Oktoba 17, 2021.
Mpiganaji anayeunga mkono serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia akikabiliana na waasi wa Houthi katika mkoa wa Marib Oktoba 17, 2021. - AFP
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa kimataifa unaoongozwa na Saudi Arabia umesema imeua waasi zaidi ya 1,600 katika mashambulizi ya anga kwa karibu wiki mbili, ikia ni pamoja na zaidi ya waasi 260 waliouawa siku hizi tatu zilizopita. Idadi hii ya vifo haijathibitishwa na chanzo huru, lakini mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi yanaendelea katika eneo hilo.

Mapigano kati ya vikosi vya waaminifu wanaoungwa mkono na serikali na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran yamekithiri karibu na mji wa Marib, ulioko katika mkoa ambao rasilimali nyingi za hydrocarbon nchini hupatikana.

Muungano umewekeza sana kwa kulinda mji huu wa kimkakati. Ni ngome ya mwisho ya serikali mashariki mwa Yemen na kuangukakwake mikononi mwa waasi ingelisababisha mgawanyiko mkubwa katika vikosi vya serikali.

Waasi wa Houthi ni mara chache kutoa idadi ya majeruhi au vifo kwa upande wao, na msemaji wao alisema Jumapili kwamba vikosi vya waasi viliwaua zaidi ya wanajeshi 500 wa serikali na kujeruhi wengine 1,200 katika mapigano karibu na Marib. Yahya Saree alitoa wito wa kuendelea kwa mapigano katika hotuba ya televisheni iliyotangazwa na kituo cha waasi cha Al-Masirah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.