Pata taarifa kuu
YEMENI-USALAMA

Mapigano yaua hamsini katikati mwa Yemen

Waasi wasiopungua 50 na wanajeshi wanaounga mkono serikali, pamoja na afisa wa ngazi ya juu, wameuawa katika mapigano katikati mwa Yemen, vyanzo vya jeshi vimesema kulingana na shirika la habari la AFP.

Mapigano yanaendelea kurindima Yemen.
Mapigano yanaendelea kurindima Yemen. - AFP
Matangazo ya kibiashara

"Afisa wa cheo cha Kanali na wanajeshi wengine 19 wameuawa katika kipindi cha saa 24 zilizopita katika mapigano dhidi ya waasi wa Houthi katika wilaya ya Al-Bayda," afisa wa jeshi la serikali amesema, akiongeza kuwa waasi 30 pia wameangamia. Ripoti hii imethibitishwa na vyanzo vingine vya jeshi. Waasi wa Houthi mara chache hutoa idadi ya wapiganaji wake waliouawa au kujeruhiwa katika mapigano.

Katika wiki za hivi karibuni, waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran walisonga mbele katika jimbo hilo. Wanapigania pia udhibiti wa mji wa kimkakati wa Marib, kaskazini mwa nchi. Vikosi vya serikali vinasaidiwa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia, jirani wa Yemen na mpinzani mkubwa wa wa Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.