Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Yemen: waasi zaidi ya 165 wa Houthi wauawa kusini mwa Marib

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen umedai Jumapili (Oktoba 17) kwamba umewaua waasi zaidi ya 165 wa Houthi katika mashambulizi mapya ya anga kusini mwa mji wa kimkakati wa Marib, ambapo mapigano yamesababisha maelfu ya kuuawa katika siku za hivi karibuni.

Wapiganaji wanaounga mkono serikali ya Yemeni wakishambulia ngome ya waasi wa Kihouthi katika mkoa wa Marib, Oktoba 17, 2021.
Wapiganaji wanaounga mkono serikali ya Yemeni wakishambulia ngome ya waasi wa Kihouthi katika mkoa wa Marib, Oktoba 17, 2021. - AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya "yameharibu magari kumi ya kijeshi na kuua zaidi ya magaidi 165" katika kipindi cha saa 24 zilizopita, umoja huo umesema katika taarifa iliyotolewa na shirika la habari la serikali, SPA.

Katikati mwa wiki hii muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen ambao unaiunga mkono serikali, ulisema kuwa zaidi ya waasi 150 wa Kihouthi waliuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanyika Alhamisi kwenye jimbo la Marib.

Waasi wa Kihouthi walianzisha tena kampeni yao ya kulitwaa jimbo la Marib, ngome muhimu ya mwisho ya serikali. Waasi hao huzungumza kwa nadra kuhusu hasara na maafa ya kivita wanayopata.

Katika taarifa yao waliyoitoa siku ya Jumanne, waasi hao walisema wako ukingoni kuuchukua mji huo. Kwa mujibu wa mmoja wa maafisa, licha ya kupoteza wapiganaji wao, waasi wa Kihouthi wanazidi kusonga mbele.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.