Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Mapigano yaongezeka kaskazini mwa Yemen, zaidi ya 60 wauawa Marib

Angalau wapiganaji 65 wameuawa katika kipindi cha saa 48 zilizopita katika mkoa wa Marib kaskazini mwa Yemen, afisa wa jeshi la Yemen amesema Alhamisi (Septemba 2). Mapigano mabaya kati ya waasi wa Houthi na vikosi vya serikali yameongezeka tangu siku mbili zilizopita.

Vikosi vya serikali, vikisaidiwa na muungano unaoongozwa na Saudi Arabaia, karibu na uwanja wa vita dhidi ya waasi wa Houthi, huko al-Kassara, karibu na Marib, Juni 28, 2021.
Vikosi vya serikali, vikisaidiwa na muungano unaoongozwa na Saudi Arabaia, karibu na uwanja wa vita dhidi ya waasi wa Houthi, huko al-Kassara, karibu na Marib, Juni 28, 2021. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Ni kipindi kipya cha mashambulizi yaliyozinduliwa mwezi wa Februari mwaka huu. Tangu wakati huo, waasi wa Houthi nchini Yemen wamekuwa wakijaribu kuteka eneo la Marib, eneo linalodhibitiwa na vikosi vya serikali katika eneo kubwa linalotawaliwa na waasi kaskazini mwa Yemen.

"Upande wa vikosi vya serikali, wanajeshi 22 wameuawa na 50 wamejeruhiwa, na kundi la waasi wa Houthi kwa upande wake, limepoteza wapiganaji 43 katika kipindi cha saa 48 zilizopita" katika mapigano kusini mwa mji mkuu wa mkoa huo, amesema afisa huyo wa serikali ambaye hakutaka atajwe jina. Waasi wa Houthi kwa upande wao mara chache sana huripoti vifo na majeruhi vinavyo wakumba katika uwanja wa mapigano.

Mashambulio ya mfululizo ya waasi wa Kishia na mashambulizi ya anga ya muungano unaoongozwa na Saudia ukisaidia vikosi vya serikali yameua mamia ya watu katika eneo hili tangu mwezi wa Februari. Waasi wa Houthi wameuzingira mji huo kwa miezi kadhaa.

Miaka sita ya vita

Katika siku za hivi karibuni, vita nchini Yemen vimeanza maafa makubwa. Mashambulio ya makombora na ndege zisizo na rubani kwenye kambi ya jeshi ya vikosi vya serikali ualisababisha vifo vya askari wengi. Watu kadhaa walijeruhiwa katika nchi jirani ya Saudi Arabia, wakati uwanja wa ndege wa kiraia ulilengwa na ndege zisizo na rubani. Waasi wa Houthi walilaumiwa kwa mashambulio hayo.

Ni miaka sita sasa tangu yemen ikumbwe na vita hii na athari zake mbaya za kibinadamu. Kulingana na Umoja wa Mataifa, ripoti hii inaonyesha makumi ya maelfu ya vifo na mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu duniani

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.