Pata taarifa kuu
YEMENI-USALAMA

Yemen: Mapigano ya Marib yaongezeka, muungano wadai kuua waasi 150

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen umesema Alhamisi hii, Oktoba 14, kwamba umewaua zaidi ya waasi 150 wa Houthi katika uvamizi mpya kusini mwa mji muhimu wa Marib.

Wapiganaji wanaounga mkono serikali ya Yemeni wanakusanyika kukabiliana na mashambulio ya waasi wa Houthi karibu na mji wa Marib Septemba 27, 2021.
Wapiganaji wanaounga mkono serikali ya Yemeni wanakusanyika kukabiliana na mashambulio ya waasi wa Houthi karibu na mji wa Marib Septemba 27, 2021. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Vita hivyo viliua mamia ya watu katika mji huo katika siku za hivi karibuni. Kulingana na Umoja wa Mataifa, tayari imehamisha makumi ya maelfu ya raia.

"Operesheni hiyo iliharibu magari 11 ya kijeshi na kuua zaidi ya magaidi 150" huko Al-Abdiya, kusini mwa mji wa Marib, muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saud Arabia ukinukuliwa na shirika la habari la Saudi Arabia la SPA umesema.

Marib, mji mkuu wa mkoa Marib, unakabiliwa na vita vikali. Ni ngome ya mwisho ya serikali kaskazini mwa Yemen, ambayo inadhibitiwa kwa asilimia kubwa na  waasi wa Houthi.

Al-Abdiya iko karibu kilomita 100 kusini mwa jiji lakini iko katika mkoa wa Marib, mkoa wenye utajiri wa mafuta na wa kimkakati kuhusiana na masuala ya kijiografia kati ya kaskazini na kusini mwa Yemen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.