Pata taarifa kuu
YEMENI-USALAMA

Yemen: Waasi 105 wauawa katika mashambulizi mapya Marib

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen umesema Jumatano kwamba umewaua waasi 105 wa Houthi katika mashambulizi mapya katika muda wa saa 24 zilizopita katika mji wa kimkakati wa Marib, unaokumbwa na mashambulizi makali ya mabomu kwa wiki kadhaa.

Kwa jumla, zaidi ya watu milioni 4 wamekuwa wakimbizi wa ndani. Kulingana na Umoja wa Mataifa, watoto na wanawake ni asilimia 76% ya jumla ya wakimbizi hao wa ndani au IDP.
Kwa jumla, zaidi ya watu milioni 4 wamekuwa wakimbizi wa ndani. Kulingana na Umoja wa Mataifa, watoto na wanawake ni asilimia 76% ya jumla ya wakimbizi hao wa ndani au IDP. - AFP
Matangazo ya kibiashara

Muungano huu unasaidia wanajeshi wa serikali kutoka kikosi cha ardhini ambao wanajaribu kuzima mashambulizi ya waasi wa Houthi dhidi ya eneo la Marib, kaskazini mwa Yemen.

Kwa zaidi ya wiki mbili, muungano huo umetangaza karibu ripoti za kila siku za waasi kuuawa, lakini takwimu hizi haziwezi kuthibitishwa na vyanzo huru na Wahouthi mara chache hutangaza hasara walizozipata vitani.

Tangu kuanza kwa mwaka 2021 kwa mujibu wa UNHCR karibu watu 80,000 sawa na zaidi ya familia 13,000 wamelazimika kuzikimbia nyumba zao na kusaka hifadhi kwingineko nchini Yemen.

Kwa jumla, zaidi ya watu milioni 4 wamekuwa wakimbizi wa ndani. Kulingana na Umoja wa Mataifa, watoto na wanawake ni asilimia 76% ya jumla ya wakimbizi hao wa ndani au IDP. 

Takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, zinaonyesha kuwa Wayemeni milioni 1.2 waliohama makazi yao wanaishi katika maeneo 1,800 ya malazi  maalum yaliyotengwa .

Jimbo la Marib ndio eneo ambalo tayari linahifadhi robo ya wakimbizi wa ndani milioni nne nchini Yemen.Kwa kuongezea, UNHCR inasema nchi hiyo inahifadhi wakimbizi karibu 130,000 na zaidi ya waomba hifadhi 12,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.