Pata taarifa kuu

Wahouthi waruhusu safari za ndege za Umoja wa Mataifa kwenda Sana'a

Baada ya kusimama kwa wiki moja kufuatia migomo ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia, waasi wa Houthi, ambao wanaongoza mamlaka ya usafiri wa anga, wametangaza siku ya Jumanne kuanza "kwa muda" kwa safari za ndege za mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa hadi uwanja wa ndege wa Sana'a.

Ndege ya shirika la kibinadamu la Umoja wa Mataifa inawarejesha mapacha wa Yemen, Mohamed na Ahmed katika mji mkuu unaodhibitiwa na waasi wa Sana'a mwezi uliopita kufuatia upasuaji uliofaulu nchini Jordan kwa kuwatenganisha baada ya kuzaliwa wakiwa wameungana mwaka jana.
Ndege ya shirika la kibinadamu la Umoja wa Mataifa inawarejesha mapacha wa Yemen, Mohamed na Ahmed katika mji mkuu unaodhibitiwa na waasi wa Sana'a mwezi uliopita kufuatia upasuaji uliofaulu nchini Jordan kwa kuwatenganisha baada ya kuzaliwa wakiwa wameungana mwaka jana. Fuad MOOHIALDIN UNICEF/AFP
Matangazo ya kibiashara

Waasi wa Houthi walitangaza Jumanne (tarehe 28 Desemba) kuanza "kwa muda" kwa safari za ndege za mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa kuelekea uwanja wa ndege wa Sana'a, baada ya kusimama kwa wiki moja kufuatia mashambulizi ya anga ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia kwenye mji mkuu wa Yemen unaodhibitiwa na waasi.

Mamlaka ya usafiri wa anga inayoongozwa na Houthi imesema katika taarifa yake kuwa inaidhinisha kurejeshwa kwa safari za ndege za Umoja wa Mataifa "baada ya hitilafu katika mawasiliano na vifaa vya urambazaji kusuluhishwa kwa muda."

"Mamlaka ya usafiri wa anga inatangaza kurejesha kwa muda safari za ndege za Umoja wa Mataifa na mashirika mengine kwenda uwanja wa ndege wa Sana'a," kituo cha televisheni cha waasi Al-Masirah kimesema. Pia mamlaka ya usafiri wa anga imetoa wito kwa shirika la Umoja wa Mataifa kuwezesha kuingia nchini Yemen vyombo vipya vya urambazaji vilivyonunuliwa hivi karibuni.

Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia ulisema ulishambulia tu maeneo ya kijeshi kwenye uwanja wa ndege, ambapo mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yalirushwa kuelekea Saudi Arabia.

Operesheni ya kijeshi "ya kiwango cha juu".

Saudi Arabia imeingilia kati Yemen tangu mwaka 2015 ikiongoza muungano unaosaidia vikosi vya serikali, katika vita kwa miaka saba dhidi ya waasi wa Houthi, wanaoungwa mkono na Iran, mpinzani wa kikanda wa Saudi Arabia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.