Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa: Kupunguzwa kwa msaada wa chakula kunakuja wakati mbaya Yemen

Umoja wa Mataifa unasema "utalazimika" kupunguza msaada wa chakula nchini Yemen kwa ukosefu wa fedha zinazohitajika. "Hatua hii inakatisha tamaa" wakati njaa inaongezeka katika nchi hii inayokumbwa vita, moja ya migogoro mibaya zaidi ya kibinadamu duniani.

Umoja wa Mataifa unabaini kwamba watoto milioni 2.3 wa Yemen walio chini ya umri wa miaka 5 wanaweza kukabiliwa na utapiamlo. Hapa ni katika mji wa Sana'a, Februari 13, 2021.
Umoja wa Mataifa unabaini kwamba watoto milioni 2.3 wa Yemen walio chini ya umri wa miaka 5 wanaweza kukabiliwa na utapiamlo. Hapa ni katika mji wa Sana'a, Februari 13, 2021. REUTERS - KHALED ABDULLAH
Matangazo ya kibiashara

Nchini Yemen, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, linatoa tahadhari. Kwa ukosefu wa fedha, shirika hili la Umoja wa Mataifa litalazimika kupunguza msaada wake wa chakula. Wayemeni milioni nane wameathirika, na kupunguzwa huku kwa msaada wa chakula kunakuja wakati mbaya zaidi. Hali ni mbaya zaidi, njaa inaongezeka siku hadi siku nchini humo. Asilimia 80 ya watu zaidi ya milioni 30 wa Yemen wanategemea misaada ya kimataifa.

Yemen, nchi maskini zaidi kwenye rasi ya Arabia, inakumbwa na mzozo wa miaka saba kati ya waasi wa Houthi, wakiungwa mkono na Iran, na vikosi vya serikali, vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia.

"Leo, kwa sababu hatuna fedha za kutosha, tunalazimika kupunguza msaada wa chakula kwa raia," Annabel Symington, msemaji wa WFP kwa Yemen amesema, alipokuwa akihojiwa na Nicolas Feldmann. Watu milioni nane sasa watapokea nusu tu ya mgao wa chakula wa kila siku. Ni lazima tufanye hivi ili kuendelea kusaidia watu wengine: watu milioni tano walio dhaifu zaidi walio katika hatari ya kukumbwa na hali ya njaa. Kwa hivyo hapa ndipo tumefikia: kupunguza misaada kutoka kwa watu wenye njaa ili kukidhi mahitaji ya wale wanaokabiliwa na njaa. Inasikitisha kufikia kwenye hatua hii. "

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa lilikadiria kuwa zaidi ya nusu ya watu wa Yemen wanakabiliwa na njaa kali na nusu ya watoto walio chini ya miaka mitano (milioni 2.3) wako katika hatari ya utapiamlo.

Wito kwa michango

WFP ilisema inahitaji dola milioni 813 (karibu euro 721 milioni) "kuendelea kusaidia walio hatarini zaidi nchini Yemen hadi mwezi Mei". Na mwaka 2022, dola bilioni 1.97 (sawa na euro bilioni 1.74) zitahitajika "kuendelea kutoa msaada muhimu wa chakula kwa familia zinazokabiliwa na njaa."

Mwezi Machi, Umoja wa Mataifa, Sweden na Uswisi ziliandaa mkutano wa wafadhili ulioshirikisha takriban nchi 100, na kukusanya karibu nusu ya fedha zilizotarajiwa kwa ajili ya misaada ya kibinadamu nchini Yemen.

Lengo la Umoja wa Mataifa lilikuwa kukusanya dola bilioni 3.85 (sawa na euro 3.4 bilioni) lakini ni bilioni 1.7 tu ( sawa na euro 1.5 bilioni) ambazo ziliahidiwa na serikali na baadhi ya wafadhili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.