Pata taarifa kuu
IRAQ-USALAMA

Iraq: Makumi ya watu wauawa katika vita dhidi ya kundi la IS karibu na Diyala

Mapambano dhidi ya kundi la Islamic State yanaendelea katika ardhi ya Iraq. Mashambulizi ya kundi hilo la kigaidi yanazidi kuongezeka katika maeneo yanayozozaniwa kati ya Kurdistan na maeneo mengine ya Iraq. Vikosi vya jeshi vimetangaza vifo kadhaa kila upande katika siku za hivi karibuni.

Bendera ya shirika la Islamic State kwenye barabara ya kuelekea kituo cha kijeshi cha al-Fatiha, kusini mwa Hawija, katika mkoa wa Kirkuk kaskazini mwa Iraq, Oktoba 2, 2017.
Bendera ya shirika la Islamic State kwenye barabara ya kuelekea kituo cha kijeshi cha al-Fatiha, kusini mwa Hawija, katika mkoa wa Kirkuk kaskazini mwa Iraq, Oktoba 2, 2017. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi kadhaa na maafisa wa polisi waliuawa katika milipuko au mapigano na vikosi vya kundi la Islamic State katika mkoa wa Diyala. Kundi la IS pia limerekodi hasara kubwa, kwa mujibu wa jeshi la Iraq.

Operesheni kubwa ya kijeshi ilianzishwa Jumapili iliyopita, Desemba 26 karibu na Milima ya Hamrin ambapo wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi wanajificha kwa lengo la kuhujumu wakaazi wa maeneo hayo na maeneo jirani nyakati za usiku. Mwaka huu, kundi la Islamic State lilifanya mashambulizi zaidi ya 200 katika maeneo yanayozozaniwa, kulingana na vikosi vya Wakurdi. Mashambilizi yalizidi katika miezi ya hivi karibuni.

Wakati huo huo, kundi hili la kigaidi linajaribu kuzua mifarakano kati ya jamii tofauti zinazoishi katika ardhi hizi zenye idadi kubwa ya watu kihistoria.

Ugumu wa kuanzisha kikosi cha pamoja

Tangu msimu wa joto uliopita, Erbil na Baghdad wamekuwa wakijaribu kukubaliana juu ya uanzishwaji wakikosi cha pamoja. Mzozo kati ya mamlaka ya Iraq na Wakurdi kuhusu umiliki wa maeneo haya daima umekuwa kwa manufaa ya kundi la kigaidi.

Brigedi hizi za pamoja zinapaswa kuanzishwa rasmi katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka wa 2022. Lakini itakuwa vigumu kwa pande hizi kutokana na uhusiano wenye utata kati ya pande hizi mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.