Pata taarifa kuu

Papa Francis ampokea rais wa Palestina Mahmoud Abbas mjini Vatican

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amekutana na kiongozi wa kanisa Katolika duniani Papa Francis na maafisa kadhaa wa kanisa hilo huko Vatican Alhamisi hii ambapo walizungumza juu ya "haja ya kuanzisha tena mazungumzo kwa suluhisho la serikali mbili" katika Mashariki ya Kati, Vatican imetangaza.

Ni ziara ya sita kwa Mahmoud Abbas kutembelea Vatican tangu Papa Francis, raia wa  Argentina, achaguliwe mwaka 2013, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Vaticannews.
Ni ziara ya sita kwa Mahmoud Abbas kutembelea Vatican tangu Papa Francis, raia wa Argentina, achaguliwe mwaka 2013, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Vaticannews. REUTERS/Alberto Pizzoli/Pool
Matangazo ya kibiashara

Kama sehemu ya hadhira hii ya faragha, Mahmoud Abbas amekutana hasa na afisa anayehusika na mambo ya nje Pietro Parolin, nambari 2 wa Vatican, na Askofu Mkuu Paul Gallagher, anayehusika na mahusiano na mataifa mengine.

Suluhisho la serikali mbili

"Haja kamili ya kuanzisha tena mazungumzo ya moja kwa moja ili kufikia suluhu ya serikali mbili, hasa kupitia juhudi kubwa zaidi za jumuiya ya kimataifa," imezungumzwa wakati wa mazungumzo haya "ya kirafiki," Vatican imesema katika taarifa.

"Imethibitishwa tena kwamba Jerusalem lazima itambuliwe na wote kama mahali pa kukutania na sio pa migogoro, na kwamba hadhi yake lazima ihifadhi utambulisho wake na tabia yake ya ulimwengu kama mji mtakatifu kwa dini tatu za Ibrahimu," taarifa hiyo imeendelea.

Ni ziara ya sita kwa Mahmoud Abbas kutembelea Vatican tangu Papa Francis, raia wa  Argentina, achaguliwe mwaka 2013, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Vaticannews. Ziara yake ya mwisho ilikuwa mwezi Desemba 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.