Pata taarifa kuu

Israeli kujenga nyumba mpya 1,355 katika Ukingo wa Magharibi

Kwa mara ya kwanza tangu kuundwa kwake, serikali ya Naftali Bennett inapinga wazi wazi Marekani kwa kutoa wito wa zabuni za ujenzi wa nyumba 1,355 katika Ukingo wa Magharibi.

Maandamano dhidi ya makazi ya Israeli huko Masafer Yatta, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israeli, Oktoba 23, 2021, wakati mpango mkubwa wa ujenzi wa makazi ya Wayahudi ulianza katika eneo linalokaliwa.
Maandamano dhidi ya makazi ya Israeli huko Masafer Yatta, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israeli, Oktoba 23, 2021, wakati mpango mkubwa wa ujenzi wa makazi ya Wayahudi ulianza katika eneo linalokaliwa. REUTERS - MUSSA ISSA QAWASMA
Matangazo ya kibiashara

Nyumba hizi mpya 1,355 zitajengwa katika makazi saba katika Ukingo wa Magharibi. Jiji la Ariel, moja wapo ya makazi makubwa zaidi, peke yake litakuwa nyumba 729.

Wizara ya Ujenzi ya Israeli pia imebaini nia yake ya kuongeza mara mbili idadi ya Wayahudi wa Bonde la Yordani na mpango wa kuuza nyumba 1,500 katika eneo hili ifikapo mwaka 2026. "Kuongeza uwepo wa Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi ni muhimu katika maono ya Wazayuni," ametangaza Zeev Elkin.

Siku ya Jumatano, kamati ya mipango ya Wizara ya Ulinzi ya Israeli inatarajiwa kutoa idhini ya mwisho kwa ujenzi wa nyumba zaidi ya 3,000 katika Ukingo wa Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.