Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA

Facebook yafunga kurasa za wafuasi wa chama tawala NRM

Kampuni ya facebook, imefunga kurasa za viongozi na wafuasi wa chama tawala nchini Uganda NRM kuelekea Uchaguzi Mkuu siku ya Alhamisi.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Kampuni hiyo ya teknolojia imesema hatua hiyo imechukuliwa ili kuwazuia viongozi wa chama cha NRM, ambao walikuwa wanataka kutumia mtandao huo kuendesha mjadala ambao ungepotosha umma kuelekea uchagusi huo.

Mkuu wa kampuni hiyo barani Afrika, Kezia Anim-Addo, aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa, hatua hiyo imechukuliwa ili kuepuka mijadili isiyokuwa na uhalisia nchini Uganda.

Hivi karibuni wafuasi wa NRM walilalamika kutokuwa na uwezo wa kuchapisha taarifa mbalimbali katika mitandao yao, hatua ambayo rais Yoweri Museveni kupitia afisa wake wa Habari Don Wanyama, ambaye pia alifungiwa mitandao yake ,  kusema kuwa hatua hiyo ni mojawapo ya mipango ya nchi za Magharibi kujaribu kjuingilia siasa za nchi hiyo.

Kampuni ya Facebook hivi karibuni pia imemfungia rais wa Marekani anayeondoka madarakani, Donald Trump,  kufuatia mchafuko yaliyotokea nchini mwake, na kuwacha maswali kuhusu nafasi ya wamili ya kamûni hiyo kuamua mauadhui ya wateja Wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.