Pata taarifa kuu
KENYA-UNSC

Kenya yaanza kuhudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Kenya imejiunga rasmi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama mwanachama asiye wa kudumu kwa kipindi cha miaka miwili ijayo, kuanzia Januari Mosi, nafasi inayotazamwa kuwa muhimu kwa mataifa ya Afrika.

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa UN Photo/Loey Felipe
Matangazo ya kibiashara

Sauti ya Kenya ambayo kwa muda mrefu, imeonekana thabiti katika ukanda wa Afrika Mashariki na pembe ya Afrika, inaangaziwa na wadadisi wa mambo iwapo itasaidia kutuliza mzozo wa jimbo la Tigray nchini Ethiopia na Uchaguzi nchini Somalia unaotarajiwa kufanyika mapema mwaka huu.

Miongoni mwa malengo ya Kenya ni kuhakikisha kuwa kundi la kigaidi la Al Shabab linaorodheswa katika kundi la magaidi na Umoja wa Mataifa kama ilivyo kwa Al Qaeda.

Kidiplomasia, Kenya inatarajiwa kutumia kiti chake kuhakikisha kuwa inashinda mzozo wake wa kidiplomasia na Somalia, kuhusu mpaka wa Bahari Hindi.

Kuhusu mzozo wa jimbo la Tigray, huenda Ethiopia itataka kuitumia Kenya kusukuma mzozo huo kuwa ajenda ya Kimataifa, wakati huu mataifa ya Ulaya yakitaka wasuluhishi wa Kimataifa kuingilia.

Aidha, katika kipindi hicho cha miaka miwili, Kenya huenda ikakabiliwa na wakati mgumu wa kuungana mshirika wake wa karibu Marekani kuhusu masuala ya usalama na China kuhusu masuala ya Uchumi, na hiyvo itakuwa ngumu kwa Kenya kuchagua ni upande upi wa kuegemea na kuingia madarakani kwa rais Joe Biden kunatazamwa kuwa huenda kukabadili upepo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.