Pata taarifa kuu
TANZANIA-UGANDA-UCHUMI

Tanzania na Uganda kunufaika kiuchumi kupitia mradi wa bomba la mafuta

Viongozi wa Tanzania na Uganda wametia saini makubaliano ya kuanzisha ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima hadi katika bandari ya Tanga.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akiwa na mwenyeji wake rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, wakati alipowasili jijini Dar es Salaam, Tanzania kwa ziara ya kikazi
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akiwa na mwenyeji wake rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, wakati alipowasili jijini Dar es Salaam, Tanzania kwa ziara ya kikazi Ikulu/Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya Uganda kugundua mafuta mwaka 2006 na kuamua mafuta hayo kupitia nchini Tanzania katika bomba la umbali wa kilomita 1,445 hadi Bandari ya Tanga ili kusafirishwa katika soko la kimataifa.

Ujenzi wa bomba hili utagharimu nchi hizo mbili Dola za Marekani Bilioni 3.5.

Rais Museveni ameelezea namna nchi hizo mbili zitakavyogawana faida ya mradi huo.

Utiaji saini wa maelewano hayo umefanyika kati ya rais John Magufuli na Yoweri Museveni huko Chato, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Haijafahamika ni lini mradi huo utaanza, lakini unatarajiwa kuchukua kati ya miaka miwili na mitatu kukamilika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.